May 8, 2013

Soda zina kemikali hatari mwilini mwa binadamu.

Soda
HAKISHA UMESOMA HII NA UMESHARE NA MWEZAKO NI MUHIMU KUPITA HATA UHAI WAKO...! 

*Utafiti wabaini ina kiwango kikubwa cha kemikali
hatari mwilini mwa binadamu AFYA za mamilioni ya Watanzania wanaotumia
vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya
kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye
kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo.

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa
Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative
Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti
zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya
ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi
aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa
binadamu.

Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali
duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa


vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.
Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la
vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa
matumizi ya binadamu. IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa
yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda
yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza
na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo
yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa
binadamu.

Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni
ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa
maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara
makubwa katika mwili wa binadamu. Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu
mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa
kupindukia ulio ndani ya soda. Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa
kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza
wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo
ndani ya soda. IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho
ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa
sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha
kikutumia kinywaji hicho. Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya
soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji
kuwa teja wa kinywaji hicho.

Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda
inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa
watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya
kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na
mengineyo. Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa
soda huwekewa ‘fructose’ (sukari) nyingi kupitia
mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo
inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene,
kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine
sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla. Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya
lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani,
amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini
humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari
kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au
zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.

Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa
kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha
kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya
kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya
mtumiaji kwa kiwango cha juu.

Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina
yoyote zaidi ya maji na sukari. Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi
mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi
hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi
kikubwa cha madini joto. Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330
husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja
kwa mwezi. Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA),
Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo
vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa
kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika
siku za hivi karibuni.

Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa
asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni
umeongezeka mara sita. “Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na
gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa
sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne
yanayomaliza Watanzania,” alisema. Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini
kwamba kati ya watu watano waathirika wa
kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya
serikali.

Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari
nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha
vimeng’enya tofauti na vyakula vingine na pia
imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye
mzunguko wa damu husababisha kongosho
kuzalisha vimeng’enya vingi mwilini. Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya
wanawake ya Boston nchini Marekani na katika
Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha
wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari
mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane
baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.

Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake
waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja
ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na
walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari. Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na
husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali
inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya
kuvunjika mifupa kirahisi.

Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na
unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama
kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo. Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa
na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali
mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.

Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza
madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa
ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini,
huvurugu mfumo wa kumeng’enya chakula tumboni
kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye
soda. Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama
kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina
madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu
hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.

Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa
tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya
kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba
ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika
mwili wa binadamu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...