Sep 10, 2013

Joseph Kaniki na Mkwanda Matumla Wanaswa na dawa za kulevya Ethiopia...


Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa nyota wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Taifa, Joseph Kaniki ‘Golota’ na bondia Mkwanda Matumla wanashikiliwa huku Addis Ababa, Ethiopia wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya.

Kukamatwa kwao kumezidi kuongeza idadi ya Watanzania maarufu waliotiwa mbaroni nje ya nchi katika siku za karibuni wakituhimiwa kwa makosa hayo.

Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili, wasanii Agnes Gerald Masogange na Melisa Edward kukamatwa kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6bilioni.

Aidha, hilo limetokea baada ya meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa na maofisa Forodha na askari wa doria wa Italia katika Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterranean ikiwa na tani 30 ya dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50milioni (Sh125 bilioni).

Aug 26, 2013

Dillish mshindi ndani ya Big Brother 2013...

Dillish 22, Namibian Lady student of Psychology.
After expressing her desires to be the first woman to win the Big Brother grand prize since Zambia's Cherise did so seven seasons ago, Dillish has done it for all of Africa's women!

The gorgeous Namibian started her Chase race as the proverbial underdog and was labeled everything from lazy, to a pampered princess. As the Chase rolled on however, Dillish quickly emerged as a very strong contender for the Chase title and won her fellow Housemates and Africa over, with her quirky, accented alter ego, aptly titled Princess Dillish.

The Namibian made sure to stay away from trouble and coasted through the Chase by taking her place behind the scenes. While her fellow Housemates got themselves into hot water, fighting and gossiping their way to what they hoped was the top of the mountain, Dillish remained grounded and maintained cordial relations with her fellow Housemates.

The only time the Namibian got herself in a spot of trouble was when she and her good friend, Nigeria's Melvin, had a disagreement after she told her fellow Housemates about a relationship he was involved in, which was less than stellar. Dillish and Cleo proved to all and sundry that women are indeed a force of nature. The two hotties pipped their male counterparts, Elikem and Melvin to the Top 2, as well as their close friend Beverly.

Before the big news was delivered, Pebbles the fish surprised all and sundry with one last speech. "On behalf of myself and the other fish, I would like to congratulate you on your amazing feat. You are the specialest ladies in Africa," Pebbles said.

However, one thing is clear! Tonight is Dillish's night and oh what a moment it was! As soon as the Namibian was announced the winner of the Chase, the Namibian broke down in a heap of tears at the realisation that she has a cool USD 300 000 sitting in her bank account. Yes Africa. She came, she saw and she conquered. In heels even! Congratulations to Delicious Dillish!

Aug 19, 2013

OFISA WA JESHI ATOROKEA RWANDA NA SIRI NZITO ZA JESHI....!!

Mkuu wa Majeshi Nchini,  Jenerali Davis Mwamunyange
*Adaiwa kutoweka na nyaraka nyeti

OFISA wa cheo cha juu katika Jeshi la Wananchi (JWTZ), anayeaminika kuwa na asili ya Rwanda, ametoweka katika mazingira ya kutatanisha, huku akiacha wingu la mashaka kwamba, hatua yake hiyo inaweza ikawa imeambatana na kupotea pia kwa baadhi ya taarifa muhimu za kijeshi.

Taarifa za kutoweka kwa ofisa huyo mwenye cheo cha luteni kanali, zinalihusisha tukio hilo na hatua za makachero wa JWTZ kufuatilia nyendo zake na zililifikia gazeti la MTANZANIA Jumapili kwa mara ya kwanza katikati ya wiki hii.

Vyanzo vya habari vya kuaminika vinaeleza kuwa, tayari maofisa wa JWTZ wameshaanza kufuatilia kwa karibu tukio la kutoweka kwa ofisa huyo, ambalo pia limezusha hali ya sintofahamu kwamba, huenda akawa ameondoka na nyaraka nyeti za kijeshi.

Kabla ya kutoweka ofisa huyo, ambaye nyendo zake zimekuwa katika darubini kali za makachero wa JWTZ, alikuwa akifanya kazi katika kitengo cha teknolojia ya mawasiliano ya kijeshi (IT).

Aug 17, 2013

Mwakyembe afumua mtandao wa ‘unga’

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu usafirishaji wa madawa ya kulevya unavyofanyika katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaa.

Dar es Salaam. Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana ameanika majina ya watu saba waliohusika kupitisha mabegi tisa yaliyokuwa na kilo 180 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh8 bilioni, Julai 5 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wakiwamo maofisa usalama wanne wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na polisi mmoja.

Alisema mizigo ikishaondoka mikononi mwa abiria hukaguliwa tena kwa kutumia mbwa wa Idara ya Usalama wa Taifa, lakini siku ya tukio hilo mbwa hao walichelewa na walitumika baada ya mizigo kuingizwa kwenye masanduku ya chuma.

“Kwa abiria watatu kuwa na mabegi makubwa tisa yanayofanana si kitu cha kawaida kukwepa jicho la maofisa wa ushuru wa forodha na vyombo vya usalama, sijui walikuwa wapi siku hiyo?” alihoji Mwakyembe.

Juzi waziri huyo aliahidi kuyaweka hadharani majina ya watu wanaosafirisha dawa za kulevya nchini, na alitekeleza ahadi hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, kusema kuwa watu hao wamenaswa baada ya mfumo wa kamera (CCTV) za uwanja huo kudaka matukio kadhaa yaliyotokea siku ya tukio hilo, kuanzia saa 9:25 hadi saa 10:30 alfajiri.

Aug 9, 2013

MADHARA YA KUPIGA PUNYETO /JE WAJUA UNAWEZA PATA CANCER??

Kujichua au kujichezea (kupiga puri au punyeto) sio kwa wanaume tu bali hata wanawake wanafanya hivyo ila wengi wao huwa hawako huru kulizungumzia au kukili kuwa wakizidiwa huwa wanajisaidia…….

Wakati mwingine mtu anashindwa kabisa kupata usingizi mpaka upige moja-mbili ndio usingizi unakuja au asubuhi unajisikia mzito kuamka kitandani mpaka upige moja ndio nguvu zinakuja…hasa kama umezoea dozi za maana lakini sasa mpenzi hayupo karibu.

Leo nitaongelea Hasara za kujichua au kujichezea kwa mwanaume.

HASARA ZA KUJICHUA KWA MWANAUME:

1. Kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi.
Athari kubwa ya kupiga puri ni kuwa hupunguza kwa kiasi kikubwa hisia za mapenzi za mwanaume na kumfanya awe mtumwa sawa na mtumwa wa pombe.

2. Huathiri mfumo mzima wa kufanya mapenzi na kumfanya apizi haraka sana ( ndani ya dakika 3 tu).


Hii inatokana na kweli kuwa mwili wako unakuwa umeuzoeza kutoa mbegu kwa dakika chache kupitia njia ya kujichua.Tambua kuwa hakuna kitu wanawake wanachukia kama kupizi mapema.

3. Humfanya mwanaume ashindwe kurudia ROUND YA PILI NA KUENDELEA....

Hakuna mwanaume anayeweza kujichua kwa round tatu mfululiza hapo hapo.... Kwa kuwa mwili unakuwa umeuzoeza kupiga round moja tu, tena fasta, ndivyo itakavyo kuwa hata ukiwa na mpenzi wako.

Amini au usiamini.Ukweli ni kwaba hutaweza kurudia round kaka!!!... Vinginevyo upewe masaa kadhaa ya kupumzika.

4. Humfanya mwanaume kuwa MTUMWA wa kujichua.

Athari nyingine ya kujichua ni kuwa humfanya mwanaume awe mtumwa. Kama alizoea kupiga puri wakati wa kulala, au asubuhi, au mchana ni lazima afanye hivyo kila siku.... Haijalishi yuko wapi.Hata angekuwa na wenzake, ni lazima atakimbilia hata chooni ili mradi afanye hivyo.

5. Humfanya mwanaume ashindwe kabisa kutoa bao.

Hii hutokea kwa mwanaume aliyezoea kupiga puri kwa miaka kadhaa.

Jamani, nafikiri mtakubaliana na mimi kuwa VIDOLE ni tofaut kabisa na Njia ya uzazi wa mwanamke. Kwanza ni vigumu na havina maji maji. Hali hii humfanya mwanaume ashindwe kupizi au kusimamisha, na hilo ni tatizo. Kwa kutumia mikono utatumia nguvu sana kujichua.

Sasa inapotokea ukafanya mapenzi live baada ya kutoka katika kipindi kirefu cha kupiga puri, mwili hushindwa kuendana na mabadiliko hayo.

6 Ni rahisi kupatwa na maradhi kama KANSA YA KORODANI.Kwa kitaalamu inaitwa PROSTATE CANCER.

Gonjwa hili hushambulia mirija ya chini ya uume na huufanya mkojo kuwa na mrundikano mwingi wa damu.

Kwa habari zingine zaidi:-

Aug 8, 2013

Wanawake waingereza washambuliwa Zanzibar.

Maji ya Acid.
Polisi katika kisiwa cha Zanzibar wamesema wanawake wawili wa Uingereza wamerushiwa maji ya Acid katika nyuso zao baada ya kuvamiwa mwendo wa usiku.

Naibu kamishna wa polisi amesema kuwa wanaume wawili waliwatendea wanawake hao kitendo hicho walipokuwa wakitembea katika barabara za mji wa kihistoria wa zanzibar.

Amesema kuwa polisi tayari wameanzisha msako dhidi yao wanaume hao.

Wanawake hao, wanasemkana kufanyia kazi shirika moja la kujitolea na nia ya shambulizi halo haijulikani.

Chanzo:- BBC

Aug 6, 2013

Ushindi wa Mugabe, Wafuasi wa MDC wadai kushambuliwa ZIM...

Ushindani ulikuwa mkali kati ya Morgan Tsvangirai na Mugabe katika uchaguzi mkuu.
Siku moja baada ya Rais Robert Mugabe na Zanu PF kutangazwa kushinda uchaguzi Mkuu nchini humo, baadhi ya wafuasi wa upinzani kutoka chama cha MDC wanasema wameshambuliwa na wenzao wa ZANU PF.

Baadhi ya dola za Magharibi ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, zimetilia shaka iwapo uchaguzi huo ulifanyika kwa uwazi.

Madai hayo yanakuja siku moja baada ya matokeo rasmi ya uchaguzi uliofanyika Jumatano kutolewa na kumpa ushindi rais Robert Mugabe.

Chama chake Zanu-PF kilipata thuluthi tatu ya viti vya bunge.

JOHN TENDWA NJE...!!

John Tendwa.
Rais Jakaya Kikwete amemteua Jaji Francis Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kujaza nafasi iliyoachwa na John Tendwa ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilisema kuwa uteuzi huo ulianza Agosti 2, 2013.

Kabla ya uteuzi huo, Mutungi ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali katika idara ya Mahakama, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Alikotoka
Historia ya Jaji Mutungi katika utumishi wake mahakamani ilianza mwaka 1989 alipoanza kazi akiwa hakimu, baadaye akateuliwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Baadaye aliteuliwa na kushika nafasi za Msajili Mahakama ya Ardhi; Hakimu Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Msajili Mahakama ya Rufani na hatimaye Jaji katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Kuhusu Tendwa
Tendwa ameachia nafasi hiyo akiwa katika msuguano wa kisiasa na baadhi ya vyama vya siasa, kikiwamo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho hivi karibuni kilitangaza kutokumtambua wala kushirikiana naye.

Katika utumishi wake huo wa miaka 12 tangu alipoachiwa nafasi hiyo na Jaji George Liundi, Tendwa amekuwa akishutumiwa mara kwa mara kwa upendeleo dhidi ya vyama vya upinzani, madai ambayo amekuwa akiyapuuza. Alipotafutwa tena jana kuzungumzia madai hayo hakupatikana kwa kuwa alikuwa nje ya nchi.

Mbali na Chadema, Tendwa ambaye amewahi kukwaruzana na vyama cha CUF na TLP, mara nyingine amekuwa akitoa tishio la kuvifuta vyama hivyo kwa kile alichodai kuwa vinachochea vurugu.

Hali hiyo ilimjengea uhasama baina ya ofisi yake na vyama vya upinzani na kuna wakati aliwahi kutajwa adui namba moja wa vyama vya upinzani na demokrasia.

Mkataba wake

DOWNLOAD NYIMBO MPYA YA HAMMER Q:- STAHIMILI "RIDDIM".

Aug 4, 2013

SITAMPA KURA YANGU EDWARD LOWASSA: DR. HAMIS KIGWANGALLA

Mh: Hamis Kigwangalla
Mbunge wa Nzega Hamis Kigwangalla amesema hawezi kumpa kura yake Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa endapo jina lake litajitokeza kama mmoja ya wagombea urais.

Kigwangalla aliyasema hayo wakati akijibu swali aliloulizwa na Fina Mango katika kipindi cha Makutano kuhusu vuguvugu la urais 2015 linaloendelea ndani ya CCM juu ya mgombea urais huku Mheshimiwa Lowassa akiwa kati ya wale wanaotajwa sana kama wagombea hasa katika mitandao ya kijamii.

"Sitompa kura  Mheshimiwa Edward Lowassa kwa sababu za msingi tu, kwamba ninakipenda chama changu na nina hakika chama changu kikija na mgombea kwenye uchaguzi mkuu 2015 ambaye ana historia ya kuhusishwa na mambo machafu kama yale ya Richmond, Dowans ambayo unayasema wewe mwenye hapa tunaweza kupata tabu sana kuomba kura kwa wananchi, lakini pia tutakuwa tumewapa hoja wapinzani wetu ya kusema kwamba tunalea ufisadi, tunaubembeleza ufisadi kwa mikono miwili" Alisema Mheshimiwa Kigwangalla huku akiongezea kuwa Tanzania aihitaji rais asiyeweza kusimamia ukweli.

Akijibu swali kuhusu mitambo ya dowans, Kigwangalla alisema haoni tatizo la mitambo hiyo isipokuwa uamuzi uliotumika katika upatikanaji wake. Katika mahojiano hayo Mheshimiwa Kigwangalla alitangaza nia yake ya kugombea urais mwaka 2025 na kuongezea kuwa 2015 anaona bado ni mapema kwake kwani anaamini watanzania bado hawajamjua Hamis Kigwangalla ni mtu wa aina gani.
Chanzo: Facebook yake.

Jul 7, 2013

Tamasha la Matumaini lafana...

Rais kikwete akifungua tamasha la matumaini leo uwanja wa Taifa jijini Dar.
Rais Kikwete akiteta na Eric Shigongo mwandaaji wa Tamasha la Matumaini.

 Rais JK akiongea na kadamnasi

Timu ya Wabunge wapenzi wa Yanga.
Timu ya Wabunge wapenzi wa Simba.
Wekundu wakiingia Uwanjani.
Yanga hao wakiingia Uwanjani.
Ngumi zikipigwa kati ya Mbunge Halima Mdee na Muigizaji Jackline Wolper. Hakuna aliyeshinde, walitoka makonde 10 - 10
Mbunge Ester Bulaya akiikataa ngumi iliyorushwa na Aunt Ezekiel (kushoto). Mshindi hakupatikana, droo ya Makonde 5 - 5.

Bongo Movie kushoto na Bongo Flava kulia wakiiimba wimbo wa taifa.
Keptaini wa Bongo Fleva H. Baba akiongoza mashambulizi.

Godi Muhokozi wa timu ya Bongo flava akishangilia goli alilolifunga katika kipindi cha kwanza. Pembeni yake ni Abdul Kiba.

Mbunge wa Sengerema Mh. William Ngeleja akimkabidhi kombe la ushindi nahodha wa timu ya Bongo Flava msanii H - Baba baada ya ushindi wa Penati 2 - 0.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...