Feb 15, 2013

Breaking News: Goldie Harvey wa Prezzo, afariki Dunia.

Prezzo akiwa na Goldie.


Yule Mwanadada mshiriki wa Big Brother Africa Star Game kutoka Nigeria na baadaye kuanza mahusiano ya kimapenzi na rapper wa Kenya Prezzo, amefariki dunia

Msanii huyo aliyeimba nyimbo ya SKIBOBO, akimshirikisha AY aliaga dunia mapema jana muda mfupi tu baada ya kurudi akitokea Marekani alipokuwa ameenda kushuhudia tuzo za Grammys.

Goldie, inasemekana aliugua ghafla na hapo hapo akafariki ktk Hospitali ya Reddington, Victoria Island, Lagos, katika mikono ya rafiki yake kipenzi Denrele.

Producer wake, Kennies Music, alisema ktk mtandao wake wa Twitter na Facebook kuwa:

"It is with heavy heart that I have to inform you all that Goldie passed this night shortly after arriving Lagos from LA. May her soul rest in the eternal peace of the Lord",


Meneja wa msanii huyo alidhibitisha habari hizi kupitia account ya twitter ya Goldie kwa kusema:
"It is with heavy heart that i have to inform you all that Goldie passed this night shortly after arriving Lagos"

Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amen.
No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...