Jan 16, 2013

WANAFUNZI WA IFM WAANDAMANA.



Wanafunzi wa Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani

Wanafunzi wa Chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM waishio maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam jana waliandamana hadi kwenye ofisi za wizara ulinzi wakidai kuchoshwa na matukio ya wizi katika maeneo wanayoishi.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanachuo hao maandamano hayo yamekuja baada ya kukithiri kwa vitendo vya wizi na udhalilishaji wanaofanyiwa ikiwa ni pamoja na kubakwa ama kuingiliwa kinyume na maumbile na majambazi.

Amedai kuwa vitendo hivyo vimeendelea kutokea mara kwa mara licha ya kuwepo Polisi na Kambi mbili za Jeshi.

"Tena wakikuvamia wanakwambia lete Komputa mpakato (Laptop), Blackberry ukikataa unaonja kipigo, then unaliwa T**o na nanihii" amesema mwanachuo huyo.

Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...