Juma Kilowoko ‘Sajuki’ enzi za uhai wake. |
Simon
Mwakifwamba (kushoto) na wadau wengine wakimsaidia Sajuki (katikati) kutoka
jukwaani baada ya kudondoka katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha
mwishoni mwa mwaka jana.
|
Msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)
amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha
waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri hivi karibuni Sajuki alikuwa
anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.
Sajuki kama ambavyo anajulikana na
wengi kwa sinema zake za kashkash alikuwa akiugua maradhi ya muda mrefu mpaka
kufikia hatua ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi.
Sajuki ambaye ameacha mjane ambaye
pia ni msanii aitwaye Wastara ambaye ni mlemavu wa mguu mmoja ambao
ulisababishwa kwa kupata ajali mnamo mwaka 2008 siku chache kabla ya ndoa. Hata
hivyo Sajuki aliamua kumuoa hivyo hivyo kwani alikuwa ameshapeleka posa kwa
kina Wastara.
Tukio hilo liligusa hisia za watu
wengi na kumchukulia Sajuki kama shujaa na mwanaume mwenye mapenzi ya kweli kwa
kitendo hicho alichokifanya.
Mwaka 2011 haukuwa mzuri kwa Sajuki
kwani ndio mwaka ambao maradhi yaliyomsumbua muda mrefu yalipamba moto
Inajulikana kuwa Sajuki aliumwa na
kufikia kipindi cha kudhoofu mwili wake kitu kilichopelekea wasanii wenzake na
watu wengine waanzishe mchango wa kumchangia Sajuki.
Waasanii, wanasiasa, wananchi
walifanikisha zoezi hilo na kumfanya aweze kwenda India kwa matibabu zaidi.
Alirudi na kuonekana kapata nafuu
kidogo jambo ambalo lilileta nyuso za furaha na amani miongoni mwa watanzania.
Hata hivyo alikuwa hajapona sawa
sawa na alikuwa anajiandaa kurudi tena India kwa matibabu zaidi.. na hii
alikiri kwenye kipindi cha 'Mkasi' kinachoendeshwa na kituo cha televisheni cha
EATV.
Sajuki ambaye ni mngoni ameshacheza
maigizo na filamu na wasanii wengi karibia wote wenye majina hapa Tanzania.
Sajuki kwa kusaidiana na mkewe
walifungua kampuni ya productions kwa ajili ya filamu (movies) za hapa
hapa nchini.
Bwana ametoa, bwana ametwaa jina
lake lihimidiwe
Source: ITV
No comments:
Post a Comment