Dec 9, 2012

MAJAMBAZI YATEKA MSAFARA WA MAITI YA MWANAFUNZI WA SUA MORORGORO!!

Gari aina ya Land Cruiser mali ya chuo cha SUA cha mjini Morogoro kama linavyoonekana baada ya kupigwa mawe na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi nje kidogo ya mji wa Singida.

Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mkoa  Singida, akirekebisha mapambo ya jeneza lililokiwa na mwili wa marehemu Munchari Lyoba, mwanafunzi wa SUA , jeneza lililovunjwa na majambazi na maiti kupekuliwa yakitafuta fedha zaidi baada ya kupora wasindikizaji.


Watu wasiofahamika idadi yao na ambao wanadhaniwa kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka Morogoro mjini hadi mkoa wa Mara na kupora  zaidi ya shilingi milioni 19.8.
Baada ya kumaliza zoezi la uporaji huo, majambazi hayo yalishusha jeneza na kisha kulifumua na kuanza kulisachi.
Jeneza hilo lilikuwa limebeba mwili wa mwanafunzi  Munchari Lyoba, mwanafunzi wa mwaka wa tatu aliyekuwa anasomea elimu ya biashara kwenye chuo cha SUA.
Amesema gari hilo lilibeba viongozi wa wanafunzi sita na viongozi wengine wanne akiwemo dereva.
Akizungumza na waandishi wa habari leo nje ya chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida, mkuu wa msafara huo Makarang  Nouna, amesema tukio hilo limetokea Disemba 6 mwaka huu saa 7.30 usiku, na lilihusisha gari Land Curise lenye namba za usajili SU 37012 na lilikuwa likiendeshwa na Kalistus Malipula.
Amesema tukio hilo la kinyamana la kusikitisha,  limetokea katika barabara kuu ya Dodoma – Mwanza nje kidogo ya mji wa Singida kwenye kona maarufu kwa jina la Mohammed Trans.
Amesema walipofika eneo la tukio, walikuta mawe makubwa yamepangwa kukatisha barabara, kitendo kilichosababisha washindwe kupita, na hivyo kutoa mwanya kuvamiwa na kundi kubwa la vijana ambao walibeba bunduki mbili aina ya gobore, marungu, mashoka na mawe.
Makaranga amesema walichofanya kwanza ni kupiga kioo cha gari letu kwa mbele, na baadaye kumparaza kwa panga usoni dereva wetu Kalistus Malipula.
Baada ya hapo walivunja vunja vyoo vyote na kutuamuru kutoa kila kitu ambacho tulikuwa nacho.
Akifafanua zaidi, amesema kwa upande wake yeye  ameporwa shilingi milioni mbili ambazo zilikuwa kwa ajili ya kugharamia msafara huo, jumla ya shilingi milioni 8.8 ambazo zilichangwa na wanafunzi  kama rambi rambi kwa  mwenzao, na shilingi milioni tisa ambazo wasindikizaji walikuwa nazo zikiwa ni posho.
“Pia tumeporwa simu  zetu zote  za mikononi, viatu, laptop na mabegi yote ya nguo zetu”amesema.
Makaranga ambaye amesema anafanya kazi za kiutawala katika chuo cha SUA, amewataja walioumizwa zaidi ni pamoja nay eye, dereva Malipula na kiongozi wa wanafunzsi Idd Idd na kutibiwa katika hospitali ya mkoa na kuruhusiwa.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, ambaye aliwasiliana na uongozi wa SUA Morogoro kwa ajili ya shughuli ya kutuma gari jingine na ukarabati wa jeneza, amesema kuwa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na kamati ya ulinzi na usalama, watahakikisha watu waliofanya unyama huo, wanakamatwa mapema iwezekanavyo ili waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...