Oct 17, 2012

WATU 29 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KUHUSIANA NA VURUGU NA UCHOMAJI MAKANISA MBAGALA.


Baadhi
ya watuhumiwa wa vurugu zilizotokea Mbagala jijini Dar es Salaam wiki
iliyoipita, wakiwa ndani ya gari la polisi walipofikishwa mahakama ya
hakimu Mkazi Kisutu jijini Oktoba 16, 2012 kwa mara ya kwanza.
Watuhumiwa 29, wawili kati yao wanawake, walisomewa mashtaka mbalimbali 
kuhusiana na vurugu zilizopelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto wiki
iliyopita, chanzo ikiwa ni baadhi ya watu wanaodaiwa kuwa waislamu,
kuandamana wakipinga mtoto mmoja kukojolea Quraan tukufu. 
Dhamana ya watu hao itaamuliwa Oktoba 30.

Add caption

Akina mama wanaotuhumiwa kuhusika na vurugu zilizotokea  huko Mbagala,
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wiki iliyopita, wakishuka kutoka
ndani ya gari la polisi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam jana. Akina mama hao ni miongoni mwa watuhumiwa 29
waliofikishwa kwenye mahakama hiyo kujibu mashtaka ya kuhusika na vurugu
za kuvamia makanisa, kuchoma, kuharibu mali na kuiba.


Watuhumiwa
wa vurugu za Mbagala wiki iliyopita, wakiwa chini ya ulinzi wa polisi. 
Polisi aliyejihami kwa bunduki na radio ya mawasiliano, akishika doria kwenye
lango la kuingilia chumba cha mahakama ambako watu 29 walifikishwa
mahakamani hapo Jumanne Oktoba 16, 2012, wakikabiliwa na mashtaka kadhaa
ya kuvamia makanisa, kuharibu,  kuiba na kuchoma mali za makanisa hayo
wiki iliyopita huko Mbagala jijini Dar es Salaam. Wote wamerejeshwa
mahabusu hadi Oktoba 30 ambapo mahakimu waliokuwa wakisikiliza kesi
hiyo, wameahidi kutoa uamuzi juu ya hatma ya dhamana. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...