Oct 17, 2012

Vurugu zazuka Zanzibar baada ya habari kusambaa kuwa kiongozi wa ‘Uamsho’kamatwa

Huyu ndiye Kiongozi wa Kundi linaloitwa UAMSHO la Zanzibar Sheikh Farid anayesadikiwa  kukamatwa huko Visiwani Zanzibar. Kundi hilo shughuli zake ni za mihadhara ya Kidini hasa ya Kiislam.

Kwa mujibu wa Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.
Katibu huyo wa Uamsho na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na sasa wanawasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.
Sheikh Farid ‘amepotea’ muda ule ule ambao inadaiwa mwenzake (Sheikh Ponda) alikamatwa (saa 5 usiku wa kuamkia leo). Juu ya sakata la Sheikh Ponda fuatilia - Sheikh Ponda akamatwa Dar!

Hata hivyo, wananchi wa hapa Zanzibar wanasema polisi, UAMSHO na serikali wangesubiri wanafunzi wamalize mitihani ya Form 4 kabla ya wao kuanza malumbano yao!

 
Habari zaidi zitafuata kadri zinavyokusanywa toka vyanzo mbalimbali
.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...