Oct 18, 2012

DKT STEPHEN ULIMBOKA AFUNGUKA KUPITIA WANASHERIA WAKE.

Dr. Stephen Ulimboka
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Stephen Ulimboka pichani, Jumatano ya tarehe 17 Oktoba ameeleza ya moyoni baada ya kutoa taarifa yake kwa vyombo vya habari kupitia kwa wanasheria wake ambao ni Shayo na Nyaroro Kichere.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa aliyekuwa anawasiliana nae kabla ya kutekwa, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande usiku wa Juni 26 mwaka huu ni Bwana Ramadhani Ighondu ambaye alidaiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ni Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Katika taarifa hiyo Dk. Ulimboka anaeleza kushangazwa na kutokamatwa mtu huyo mpaka sasa na kudai kuwa yeye yupo tayari kutoa ushirikiano kwa tume huru japo mpaka sasa haijaundwa. 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...