Jul 23, 2012

Ukimwi usiosikia dawa waongezeka Afrika.

Dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi

Aina ya ugonjwa wa ukimwi ambao hausikii dawa umekuwa ukiongozeka katika bara la Afrika katika muda wa muongo mmoja uliopita.

Kwa muujibu wa ripoti iliyoandikwa na wataalamu katika jarida la kisayansi la Lancet, hali hii imebainika baada ya watu 26,000 walio na virusi hivyo kufanyiwa utafiti.
Wataalamu hao wanasema kuwa hali hiyo ya ugonjwa kutosikia dawa huenda ikatokea ikiwa wagonjwa hawatazingatia na kutumia dawa walizopewa na pia ufuatiliaji mbaya.
Shirika moja nchini Uingereza limesema kuwa hali hiyo inazusha hofu zaidi katika bara la Afrika ambapo njia mbadala ya kuwatibu wanaouguwa maradhi ya Ukimwi hakuna.
Watatifi hao kutoka shirika la Afya duniani-WHO na chuo kikuu cha University College London wamegundua kuwa aina ya ukimiwi ambao hausikii dawa unapatikana zaidi nchi za Afrka Mashariki.
Wataalam hao wanasema asilimia 26 % ya waathirika wako katika hali hiyo ikilinganishwa na asilimia 14 katika nchi zilizo kusini mwa Afrika.
Lakini katika mataifa ya Kusini mwa Marekani , Afrika Magharibi na kati hali kama hiyo haipatikani.
Akizungumza na BBC Dr Ravindra Gupta wa shirika la UCL alisema: " virusi hivyo ambayo havisikii dawa ni kwa sababu wagonjwa hawatumii dawa ipaswavyo".

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...