Baadhi ya dawa za
kukabiliana
na makali ya Ukimwi.
|
Huenda wagonjwa wa Ukimwi wakanufaika na dawa
mpya ambayo itawawezesha kutumia tembe moja kwa siku. Hii ni kwa mujibu wa
utafiti mpya nchini Marekani.
Jarida la Afya Lancet limesema tembe hiyo
inajumlisha dawa zote nne zinazokabiliana na makali ya ukimwi na kwamba ni
salama.Utafiti unasema hii itawarahisishia wagonjwa katika kuhakikisha
wanafuata maagizo ya madaktari wao.
Ukimwi hauna tiba lakini watafiti wameweza
kutoa dawa za kukabiliana na maradhi nyemela.
Watafiti pamoja na kampuni za dawa
wamechanganya dawa nne na kutengeneza tembe moja ili kurahisisha utumizi wa
dawa hiyo miongoni mwa wagonjwa.
Tembe inayofanyiwa majaribio na ambayo
imechanganywa dawa nne inauwezo wa kudhibiti virusi vya HIV kuongezeka mwilini.
Paul Sax mtafiti mkuum katika Hospitali ya
Wanawake ya Brigham huko Boston,Massachussetts ambaye pia ni mwanazuo wa ziada
wa taasisi ya afya ya Harvard ameelezea umuhimu wa tembe hii kwa kuimarisha
afya ya wagonjwa.
Dk. Sax ameongoza utafiti huu ambapo pia
wamefanyia majaribio tembe hii kwa wagonjwa 700 na kusema inafanya kazi, japo
kulitokea matatizo ya figo miongoni mwa waliotumia.
Licha ya mafanikio ya sasa watafiti wanasema raia wengi
hawafahamu hali zao ambapo wameendelea kuishi na maambukizi bila kujua.
No comments:
Post a Comment