Jul 8, 2012

PAMBANO LA FRANCIS CHEKA NA JAPHET KASEBA. JULY 7, 2012Bondia Francis Cheka aligoma kupanda kwenye stage kwa ajili ya pambano na Japhet Kaseba kwa kudai kwamba hawezi kucheza na mtu alie chini ya kiwango, aliyasema hayo pamoja na kwamba alikubali kucheza pambano, hapa kuna utata kidogo…
Bondia Japhet Kaseba na wapambe wake wakimwangilia Cheka wakati anaukimbia ulingo.
Bondia Japhet Kaseba amepewa ushindi katika mpambano wake dhidi ya Francis Cheka aliyegoma kupanda ulingoni. Cheka aliingia ulingoni lakini hakuweza kupambana na mpinzani wake badala yake alishuka na kutokomea.
     


Francis Cheka (mwenye T-sheti nyekundu) akitoka ulingoni baada ya kushindwa kupambana na Kaseba.

Pamoja na Japhet Kaseba kutangazwa mshindi kutokana na Cheka kugoma kupanda ulingoni, Cheka alizunguka uwanja kidogo huku akishangiliwa..
Japhet Kaseba wakati anatoka uwanjani kwenda vyumbani mashabiki wa jukwaa la kwanza kushoto mwa lango kuu walimtupia chupa za maji zisizopungua sita pamoja na kumzomea.

1 comment:

  1. Cheka n mshirikina ndo mana kaogopa kupgana.

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...