Jul 5, 2012

MASHUJAA BAND YAPUNGUZA WANAMUZIKI/WAFANYAKAZI KATIKA BENDI YAKE.


======TAARIFA RASMI=====

Wadau wetu tunawajurisha rasmi kuhusu upunguzaji wa wanamuziki/wafanyakazi katika bendi yenu ya MASHUJAA BAND;tunaomba mchukue taarifa hii ndiyo rasmi na siyo ambayo mmeisikia kutoka kwa wengine amabao wamejipa usemaji wa mashujaa band; Mashujaa band katika kuhakikisha inawapatia watanzania burudani iliyokusudiwa na pia kutoa maslahi bora kwa wafanyakazi wote;Ndugu wadau bendi hii tangu imeanzishwa imekuwa na kundi kubwa sana la wafanyakazi na kwa kwelli wamekuwa wanafanya kazi nzuri;lakini baada ya research ya muda mrefu tumeamua kufanya marekebisho katika kila idara na kupunguza wafanyakazi kwa awamu mbili,awamu ya kwanza ni kutoka wafanyakazi 41 mpaka 30,na awamu ya pili ambayo itafuata ndani ya miezi 3 mpaka 6 ijayo ni kutoka wafanyakzai 30 mpaka 25.Lengo ni kuwa na kikundi chenye kukidhi matarajio kwani pia kuwa na kikundi kidogo kinaleta urahisi wa kukiongoza kiutawala na kimaslahi na zuri zaidi ni rahisi kwa wafanyakazi wenyewe kushikamana na kuzoeana kirahisi ili kuleta tija katika lengo letu la kuwapa watanzania burudani nzuri.
Hivyo juzi tuliwapunguza wafanyakazi 11 kama ifuatavyo: 
muimbaji mmoja,rapper mmoja(mirinda nyeusi),mbeba vyombo mmoja,mafundi mitambo wawili,wacheza show wa kiume watatu,wacheza show wa kike watatu. Hivyo tumepunguza katika zile idara ambazo kwa maoni ya wengi ilikuwa ni zaidi ya mahitaji,na tunategemea kupunguza tena wengine watano ndani ya miezi 3 hadi 6 ijayo.Zoezi hili lilikuwa wazi na wafanyakazi wote waliambiwa mwezi mmoja uliopita kuhusu ujio huu wa hili zoezi.Vigezo vilivyotumika ni uwezo wa kikazi,na masuala ya kinidhamu. Napenda pia kuwajulisha wadau wetu kwamba hakuna hata mwanamuziki mmoja alietoka bendi fulani ambayo mkurugenzi wao jana alijitokeza na kuwa msemaji wetu eti tunampa mzigo kwani tumewafukuza kazi wanamuziki ambao tuliwachukua kwa pesa nyingi toka katika bendi yake na sasa wameenda kumlilia.Huu ni uzushi na unalenga kutujengea picha mbaya kwa jamii na hata kwa wanamuziki wote.Kupenda kuongea ongea na kupenda kuonekana katika vyombo vya habari imekuwa ndiyo mbinu ya mkurugenzi huyu na amesahau kwamba watanzania wa karne hii siyo wale miaka ile,hawadanganyiki.


=====ASANTENI SANA=====


Imesomeka ktk ukurasa wao wa Facebook.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...