Jul 8, 2012

PAMBANO LA JACKLINE WOLPER NA WEMA SEPETU, UWANJA WA TAIFA, JULY 7, 2012

Jackline Wolper akiwa ameingia uwanjani kwa mbwembwe na kuongea kwa hali ya kutamani pambano lianze mapema apigane na Wema Sepetu, Ulikua ni usiku wa tamasha la matumaini uwanja wa Taif ambapo pambano kati ya Wema na Wolper halikua kama ya mabondia wengine, wao walifanya kama kichekesho ambacho mwisho wa siku walikubali kwamba  mpambano wao ulitumika pia kuwaonyesha watanzania kwamba wawili hao hawana beef.

Wema akiwa anaingia uwanjani kwa mbwembwe huku akiahidi ushindi mapemaa!!

Refa akiwap maelekezo tayari kwa mpambano.
Yani ungekuwepo hapa ungecheka tu, kila mtu alikua anacheka.. ilikua safi sana!
Ha ha ha haaaa!!! Hapa Wema pamoja na mikwara yote aliona Jack anamletea ngumi yenye ujazo akaamua kukimbia huku akipiga kelele za kutaka aokolewe, mwishowe alikwenda kumkumbatia refa.
Pambano lilikua la round mbili tu ambapo refa alitangaza kwamba wote wametoka droo, hakuna aliemzidi mwenzake.
Wakionesha Upendo na Amani katika pambano lao.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...