Mh. Hamad Masoud Hamad. |
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Baraza la
Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee ilisema tayari
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein
amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.
“Tarehe 20 Julai, 2012 Waziri wa Miundombinu
na Mawasiliano Mheshimiwa Hamad Masoud Hamad alimuandikia barua Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohammed Shein ya
kumuomba ajiuzulu kufuatia ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit iliyotokea
Julai 18,2012” Ilisema taarifa ya Dk. Mzee.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais Dk
Shein amemteua Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani(CUF) Rashid Seif Suleiman kuwa
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano.
“Kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa
Miundombinu na Mawasiliano,Rais amemteua Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri wa
Miundombinu na Mawasiliano” Taarifa ya Ikulu ilisema.
Uteuzi wa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano
umeanza Julai 23 mwaka huu.
Wakati huo huo, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya
kuchunguza ajali ya kuzama kwa meli ya Mv. Skagit.
Mwenyekiti wa Tume hiyo ni Jaji Abdulhakim Ameir Issa,
wajumbe ni Meja Jenerali S.S. Omar, COMDR. Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla
Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu
Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla
Katibu wa Tume.
No comments:
Post a Comment