Jul 18, 2012

BREAKING NEWS: MV Seagul (SKAGIT) imezama Zanzibar.

Meli iliyokuwa imewabeba takriban watu miambili imethibitiswa kuzama katika bahari ya hindi eneo la Chumbe Mnara karibu kabisa na bandari ya Znz. Meli hiyo kwa jina SKAGIT ilikuwa inatoka Dar es Salam kuelekea Zanzibar katika safari zake za kawaida majira ya saa 6 na nusu mchana, mpaka jioni watu 150 wameripotiwa kujiokoa na kuokolewa kwa msaada wa watu mbalimbali waliowahi kufika katika eneo la bahari ilipotokea ajali hiyo.

Habari zilizotufikia Usiku huu nikuwa zoezi zima la uokoaji limesitishwa mpaka kesho na itafahamika kama kuna watu watakuwa wamepoteza maisha pamoja na idadi kamili.Bot ya Skagit ikizama na kupotea kabisa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...