May 25, 2012

Waliokufa katika ajali ya Mbunge Selasini waongezeka, wamefikia wanne akiwamo mamake!

Ni kweli. Mbunge Joseph Selasini kapata ajali eneo la Bomang'ombe Mjini, karibu na pale wanapouza nyanya... May 25, 2012 Jioni.

Chanzo cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendokasi pamoja na Gurudumu moja la mbele la gari alilokuwa akisafiria lilipasuka baada ya gari hilo kuingiliwa na pikipiki mbele na kukosa mwelekeo. Gari likaacha njia likaangukia darajani. Kwa wale wanaofahamu eneo hilo kuna daraja maarufu linaitwa Daraja la Mjapani.

Alikuwa akitokea Arusha kumtoa baba yake hospitalini. Yeye na Baba yake wamesalimika. Walikuwa wamefunga mikanda. Ndiyo iliyowasaidia. Majeruhi kwenye ajali hiyo ni pamoja na Mkewe Mbunge, Digna Kavishe (43) ambaye amepata majeraha sehemu za kichwa na hali yake siyo nzuri,

Waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni pamoja na Mama Mzazi wa Mbunge huyo, Catherine Joseph Selasini (80), Agatha Jerome Mahoo (85) mkazi wa Rombo ambaye ni mkulima pamoja na wanawake wawili ambao hawajatambulika majina yao mmoja akikadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 - 75 na mwingine 35 - 40.
 
Mbunge  Joseph Selasini ambaye alipata majeraha kwenye bega pamoja na mkono wa kulia na hali yake inaelezwa kuwa inaendelea vizuri. Alilazwa Hospitali ya Wilaya ya Hai, Baadae walihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa uchunguzi zaidi.

Miili ya Marehemu imehifadhiwa kwenye hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya taratibu za mazishi.
___________________________


HILI NDIO GARI ALILOPATA NALO AJALI MBUNGE WA ROMBOMH. JOSEPH SELASINI.
Joseph Selasini na familia yake walikua wakitokea Arusha kwenye msiba wa kiongozi mmoja wa kanisa katoliki ambapo Polisi Kilimanjaro pia imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...