May 27, 2012

VURUGU ZANZIBAR ZAENDELEA TENA LEO, WACHOMA MOTO KANISA PAMOJA LA GARI LA ASKOFU.!!

Waandamanaji wa kiislam Zanzibar wakiwa kwenye maandamano wakati wakielekea kituo cha polisi na kabla mabomu ya machozi hayajaanza kulipuliwa na askari.
Waumini dini ya kiislamu wakiwa ktk maandamano mjini Zanzibar.

 

Hizi ni baadhi ya vurugu zilizotokea jana Mjini Zanzibar huku mabomu ya machozi yakirindima na kuendelea kupigwa na polisi wakati wa vurugu zilizosababishwa na kundi kubwa la watu kwenda kuvamia kituo cha polisi ili kushinikiza kiongozi wao aliyeshikiliwa na jeshi la polisi aachiwe huru.
Askari wa kutuliza ghasia akiwa tayari kwa mapambano na waandamanaji mjini Zanzibar ambao inasemekana walivamia kituo cha polisi wakiwa na silaha za jadi kama vile rungu na mapanga.
Hali tete bado inaendelea asubuhi ya leo mjini zanzibar huku polisi wakiwatawanya wananchi wa zanzibar lakini wananchi hao wanazidi kuongezeka kwa kutaka kiongozi wao kuachiwa huru na polisi ambapo alikamatwa jana na wananchi hao kuvamia kituo cha polisi jana jioni na hatimaye polisi kutumia mabomu ya machozi tokeaa jana jioni hadi asubuhi ya leo.
Mwandamanaji wa Kiislamu Zanzibar akionyesha kitambaa chenye damu.
_______________________________

JANA JIONI KUNDI KUBWA LA WATU WANAOLIUNGANISHA KUNDI LIFAHAMIKALO KWA JINA LA UAMSHO,AMBALO LIMEKUWA LIKIUPIGA VITA MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR, LILIVAMIA KITUO KIKUU CHA POLISI CHA MADEMA KISIWANI HUMO JIONI YA JANA NA KUSABABISHA VURUGU KUBWA WAKITAKA KUACHILIWA KWA KIONGOZI WAO ALIEKAMATWA JIONI YA JANA KWA KUONGOZA MHADHARA BILA YA KUWA NA KIBALI CHA SERIKALI.
HALI HIYO IMESABABISHA VURUGU KUBWA KITUONI HAPO HUKU ASKARI POLISI WA KITUO HICHO WAKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI ILI KUWATAWANYA WATU HAO AMBAO WENGI WAO WAKO NA SILAHA ZA JADI AMBAZO NI MARUNGU,MAPANGA NA MAWE ILI KUPAMBANA NA ASKARI POLISI KITUONI HAPO VURUGU HIZO ZIMEENDELEA TENA ASUBUHI YA LEO AMBAPO WAMECHOMA MOTO KANISA PAMOJA LA GARI LA ASKOFU WA KANISA HILO.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...