May 5, 2013

Mlipuko mkubwa umetokea katika kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasisi Arusha.

CHANZO KINASEMA, BOMU HILO LIMELIPUKA WAKATI WAUMINI WA KANISA KATOLIKI WAKIENDELEA NA SHEREHE ZA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA NA MPAKA SASA HAIJAWEZA KUJULIKANA IDADI KAMILI YA WATU WALIOJERUHIWA LAKINI TAARIFA ZINASEMA KUWA KUNA BAADHI YA WATU WAMEJERUHIWA NA KUWAHISHWA HOSPITALI KWAAJILI YA MATIBABU NA MPAKA MUDA HUU HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA BOMU HILO.

CHANZO CHA BOMU HILO INASEMEKANA KUNA GARI AINA YA HIACE ILIFIKA KANISANI HAPO NA KUSIMAMA BAADAE AKASHUKA MTU ALIYEKUWA AMEVALIA VAZI MITHILI YA KANZU NA KURUSHA BOMU HILO.


BALOZI WA PAPA NCHINI NDIYE ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA NA AMENUSURIKA KATIKA BOMU HILO ILA WATU WENGI WAMEJERUHIWA.


MPAKA SASA MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA POLISI AKIHUSISHWA NA TUKIO HILO!.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...