Mar 10, 2013

Timu ya Passio FM "Passion FC" imetoa dozi kwa Majohe Veterani...

Timu ya Passion "Passion FC"
Timu ya Passion FM "Passion FC" imetoa dozi kwenye Mechi ya kirafiki na Timu ya Majohe Veterani baada ya kuipiga bao mbili kwa Moja (2 - 1) katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majohe Jumamosi ya tarehe 9 Mach.

Mchezo ulikuwa mzuri na wakuvutia ambapo wananchi wa Majohe walijaa Uwanjani kwa ajili ya kushuhudia mechi pamoja na kukutana na watangazaji wa vipindi mbalimbali vya Passion FM.

Timu na uongozi wa Passion FC unatoa shukrani nyingi na za pekee kwa Uongozi mzima wa Majohe Veterani kwa mapokezi mazuri waliyoifanyia timu hiyo.

Zifuatazo ni baadhi ya Picha za  mechi huko Majohe.

Majohe Veterani


Mashabiki walijaa.
Benchi la Ufundi Passion FC...


Mapumziko, Full Vinywaji huku uwingi wa mashabiki ukiongezeka!!
Mdau Mkubwa wa Passion FC na muandaaji wa Pambano hili (Wa pili kulia) akitoa machache pale alipokuwa akizungumza na Timu hizo baada ya mchezo.

Mchezaji machachali wa Passion FC (Kulia) Ben Mwanantal akichukua picha ya pamoja na mashabiki wa wake!!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...