Nov 6, 2012

UCHAGUZI MAREKANI.

Barack Obama v/s Mitt Romney.Wamarekani kuhitimisha upigaji kura Jumanne leo.

Rais wa Marekani Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney siku ya jumatatu walifanya kampeni za dakika za mwisho kwa wapiga kura katika majimbo muhimu.

Wagombea wawili wakuu katika mashindano hayo rais Barack Obama na mrepublican Mitt Romney walisafiri katika majimbo kadhaa yenye ushindani mkubwa katika kampeni zao za kufa na kupona kwaraia wapiga kura kujitokeza kwa wingi, kwa vile uchunguzi wa maoni unaonesha wako sare katika kinyan’ganyiro hicho.
Kufuatana na wachambuzi wa mambo mshindi atamuliwa kutokana na idadi ya watu watakao jitokeza leo na nani atakae ibuka mshindi katika majimbo saba yenye ushindani mkubwa, kwani katika uchaguzi wa Marekani rais huchaguliwa na wajumbe wa majimbo 50.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...