Nov 20, 2012

BREAKING NEWS: WANAJESHI WATATU WA JWTZ WALIOMUUA SWETU FUNDIKIRA WAHUKUMIWA KUNYONGWA.


Hayati Swetu fundikira
Watuhumiwa wakiwa mahakamani kabla ya hukumu kusomwa. kutoka kulia ni Rhoda Robert, Ally Gube na Mohamed Ally


Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imetoa adhabu ya kunyongwa wanajeshi watatu waliokuwa wakishitakiwa na kesi ya  kumuua mtoto wa Chifu Abdallah Fundikira, Swetu Fundikira kwa kukusudia.

Adhabu hiyo imetolewa mapema leo baada ya kuwakuta na hatiani washitakiwa wote watatu kwa mashitaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Wanajeshi hao ni Sajenti Rhoda Robert (42) wa  Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Mbweni,Koplo Ally Ngumbe (37) wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kikosi cha Kunduchi na Koplo Mohamed Rashid. 

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Zainabu Mruke ambaye alisikiliza kesi hiyo.

Katika hukumu yake Jaji Mruke alisema kuwa imethibitika kuwa washitakiwa waliua kwa kukusudia.

Mi dhahir hakukuwa na shahidi wa moja kwa moja washitakiwa waliua lakini mazingira yanaonesha Swetu aliuawa na washitakiwa hao.

Ni wazi upande wa mashitaka umeweza kuithibitishia mahakama pasi na shaka yoyote kuwa washitakiwa walitenda kosa la mauaji ya kukusudia.

Swetu aliuawa kutokana na majeraha yaliyotokana na kupigwa kitu kichwani hilo lilithibitishwa na Daktari ambaye ni wa Hospitali ya Taifa Muhimbili aliyetoa ushahidi kuwa alifanyia uchunguzi mwili wa marehemu.

Kwa mujibu wa ushahidi Januari 23 mwaka huu, Swetu alikutana na washitakiwa katika makutano ya barabara ya Kawawa na Mwinjuma ambapo baadaye wanajeshi hao walimchukua wakidai kuwa wanampeleka kituo cha polisi cha Osterbey lakini hawakumpeleka huko alikutwa usiku wa manane eneo la msikiti wa Jamatini Upanga akiwa na washitakiwa katika hali mbaya mpaka mauti yalipomkuta katika hospital ya Taifa ya Muhimbili.

Hata hivyo hawakufanya hivyo na baadaye walikutwa katika eneo la msikiti wa Jamatini huku mwili wa marehemu ukiwa umelala kifudifudi hauna nguo yeyote zaidi ya soksi ya mguu wa kulia ambapo katika utetezi wao walidai kuwa Swetu alivua nguo mwenyewe na kujirusha kwa kuwa hakutaka kupelekwa polisi.

Kitu cha kushangaza, Swetu alikutwa akiwa hana nguo hata moja isipokuwa soksi ya mguu mmoja akiwa amelala chini barabarani akitokwa damu kichwani na mdomoni. Katika kujitetea washitakiwa hao walidai kuwa Swetu alivua nguo mwenyewe na kwamba alijirusha kutoka kwenye gari wakimpeleka kituo cha Polisi Kikuu.

Washitakiwa walishindwa kutoa maelezo ya kutosha kuhusu kifo cha Swetu kwasababu ni wao waliondoka nae akiwa katika hali ya uzima na ni wao walikutwa nae akiwa hoi hajitambui na baadaye kufa.

Kama ambavyo inafahamika adhabu ya kunyongwa ni adhabu kubwa, ndugu wa washitakiwa hao walilia mahakamani baada ya kusomwa hukumu hiyo huku wengine wakizimia. Hata hivyo wakili wa washitakiwa hao Ruge Kalori hakuridhishwa na hukumu hiyo alisema kuwa anatarajia kukata rufaa.…ilikuwa ni saa ya majonzi na huzuni


....mmoja wa ndugu wa Fundikira akibebwa mara baada ya kuzimia na kudondoka sakafuni Add caption

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...