Jul 12, 2012

Solo Thang – Miss Tanzani, Video na MistariVideo mpya kutoka kwa Solo Thang, pata mistari yake hapo chini:
[Ubeti wa Kwanza]
Baba yake alikuwa mkoloni kipindi huyu Miss mwali
Mchonga alikata utepe lakini hakuvinjari
Sababu alikua busy kumlinda na geti kali
Kumbe wenzake wanabinjuka, kushtuka akakaa mbali
Demu alikua na heshima kabla haijatangazwa Rukhsa
Chukua Chako Mapema ukimkonyeza tu umegusa
Ana kifua kimebetuka sio maziwa ni madini
Kayaacha wazi, watu wanashika hapo ndio anaponiudhi mimi
Watu wanagonga tu Ikulu tena kwa mitindo huru
Kavu kavu bila kinga hajali vinavyodhuru

Kawa shangingi na amedata hana uwoga wa kunguru
Anapenda sana chapaa haimtoshi kodi na ushuru
Ana kijungu matata laini kama nyanya masalo
Anatingisha Afrika nzima na mzigo Kilimanjaro
Usimchezee kwa vidani sio pete sio hereni
Anamiliki tanzanite kama ardhi ya Mererani
Sura dhahabu inaita kama amezaliwa Geita
Tatizo ndio kicheche kila mwanaume ndio amepita
Hata Benja hakutoka Kapa huyu demu hajatulia
Kama rushwa ndio kikwapa ananuka na kunukia
[Kiitikio]
Miss Tanzania
Nakupenda ila hujatuliaa
Vitendo vyako sitojivunia
Sifa yako kubwa umefulia
Miss Tanzania
[Ubeti wa Pili]
Bora angebaki kuwa modo kama Flavian Matata
Ila demu amejiachia kisa anaendekeza bata
Sitachoka kuwakilisha jinsi anavyoniacha hoi
Juzi juzi kaopolewa na Handsome Boy
Kabla hapo shoga zake wote kashawaona mabwege
Sababu hawana dira na yeye ameshahongwa ndege
Anafaa kuwa Miss Dunia maandalizi longolongo
Tatizo anakula sana akijamba ni Songosongo
Mara ghafla kanenepa kumbe mimba B.O.T.
Kumbe demu aligawa EPA watu wamepiga hafu jii
Alizugwa na akaunti hewa kuwadi Bwana Bilal
Mara mdomo naye kazimwa bila hata picha ya kaburi
Kinachomponza huyu shawty utulivu sifuri
Ila hakuna anayepinga kwamba huyu demu ni mzuri
Mixer siasa na biashara demu ameshakuwa chotara
Mishe za Dar akimaliza Mjengoni anakwenda lala
Kadri miaka inavyokwenda demu anazidi fulia
Kumbe weupe ni mkorogo ona mwili sasa umefifia
Demu kazidi umalaya wacha mabwana wamteme
Haogopi kuliwa mtungo kisa nagawa umeme
[Kiitikio]
[Ubeti wa Tatu]
Wadaku walishamfuma anakula denda na Richmond
Dowans akazidi kete akamvisha pete ya diamond
Binti masikini akanasa bwana mshenga ndio Lowasa
Shemeji hataki hata picha ndio tabia gani sasa
Ndoa ilifungwa kwa vifijo vigogo wakala pizza
Keki nzima wale wao share yetu si ni giza
Sio hayo demu ana mengi ya kuchukiza
Malighafi ashazinadi for sale anajiuza
Mtaani ilivuma rumor demu kawa mama huruma
Uchumi umefungwa drip maendeleo ndio kali homa
Mali asili ndio kitasa kila ufunguo ndio unapita
Toka alipovunja ungo nusu karne imeshapita
Mapenzi kafanya mradi anamegwa na mafisadi
Amani kwa time bomb binti amekumbatia radi
Vitendo vyake vibaya vinafanya adharaulike
Tabia Katiba sio Msahafu ndio useme isibadilike
Mikosi inayomkuta ndio kwanza anatabasamu
Hajali waliomzunguka kama nao binaadamu
Mbagala walimbaka mpaka akamwaga damu
Na juzi Gongo la Mboto kaanza kujamba mabomu
[Kiitikio]

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...