Jun 14, 2012

WACHAWI WANASWA KANISA LA UFUNUO MWANZA

Chungulia mahojiano na wachawi hao wanaoshikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mwanza katika video.

Hii habari ilitokea May 20, 2012. Isome ...



Watu wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma (mwanaume) waliotambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kubanwa na kujitambulisha wamekamatwa majira ya saa 12 asubuhi leo katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa kwaajili ya sadaka.

Habari za namna hii zinatokea mala nyingi sana Nchini kwetu, na kama zinatokea mala kwa mala Serikari inasubiri nini kuamini kuwa Uchawi upo? Au neon UCHAWI lina maana gani! Na kama tatizo ni neno UCHAWI kwanini wasitafute jina jingine ili hawa watu waweze kuchukuliwa hatua za kusheria pindi wanapopatikana wakiwanga!! (na Sheria zake zitungwe…!).

Vitu vinaonekana kabisa (LIVE) na wenyewe (Wachawi) wanakili na hicho wanachokifanya ya kuwa ni UCHAWI kwa ajili ya kuua (Kutoa kafala) Binadamu wenzao.

Haya ni maoni yang utu, lakini huo pia ndo ukweli halisi…!

Watu hao wawili ambao ni Masaganya Kalimanzila umri wa miaka 30 (mwanamke) na Chiza Juma (mwanaume) waliotambulika kuwa ni wachawi mara baada ya kubanwa na kujitambulisha wamekamatwa katika kanisa la Ufunuo lililopo maeneo ya Butimba jijini Mwanza wakisafiri kwa ungo toka kijiji cha Kaziramkunda wilayani Kasulu mkoani Kigoma hadi jijini Mwanza kwania ya kuwachukuwa watu watatu walioagizwa kwaajili ya sadaka.
Abigaili Zumaridi wa kanisa hilo Ufunua akisimulia kilichotokea.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...