Diamond akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason.
|
SIRI
imefichukua kuwa madai kwamba ‘kichaa’ wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa
‘Diamond Platnumz’ ni memba wa jamii ya siri inayodaiwa kumwabudu shetani,
Freemason a.k.a Wajenzi Huru zilianza kitambo lakini sasa zimeshika kasi baada
ya kunaswa kwa picha inayomuonesha akisalimiana na mtasha kwa ishara ya
Kifreemason, Ijumaa Wikienda linaibumburua.
Kwa mujibu picha hiyo, tukio hilo
lilijiri nchini Uingereza, mwaka jana, Diamond alipokwenda huko kwa ajili ya
shoo.
MAVAZI
Ilidaiwa pia kuwa mavazi ya Diamond (meusi) yalishabihiana
sawia na yale ya mtasha huyo yanayoelezwa kuwa sehemu ya mavazi ya jamii ya
Freemason.
ISHARA
Kingine kilichoibua maswali ni ishara ya salamu ya wawili hao
ambayo ilitengeneza nembo ya Freemason ya ‘V’ au bikari kwa namna walivyogusana
kwa vidole.
Kwa mujibu wa wadau walioiona picha hiyo iliyonaswa kwenye mtandao
wa Twitter, Diamond amekuwa na ishara nyingine nyingi za aina hiyo hivyo kuzidi
kuzua utata kama ni memba wa jamii hiyo.
“Lakini inawezekana kwa sababu nasikia
ukishajiunga unapata mafanikio ya ghafla. ‘So’ kuhusu hili, sina upande wa
kusimamia,” ilisomeka sehemu ya maoni kwenye mtandao huo baada ya kuibuka
mjadala mzito juu ya ishu hiyo inayozidi kushika kasi mithili ya moto wa kifuu.
“Tungeshukuru
kama Diamond mwenyewe angejitokeza aseme ukweli kwani akinyamaza anazidi
kutuweka njia panda,” ilisomeka sehemu nyingine ya maoni hayo huku ikiungwa
mkono na wengi.
Diamond akisalimiana na mtasha kwa ishara ya Kifreemason.
|
UNATAKA KUMSIKIA DIAMOND? SOMA HAPA
Ili kumaliza utata wa je,
Diamond ni Freemason au la, Ijumaa Wikienda lilibeba jukumu la kumtafuta ili
aanike ukweli wake ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Unajua mwanzoni nilikuwa
sikumbuki ni lini na wapi nilipiga picha ya dizaini hiyo. ‘Anyway’, isiwe kesi,
nakumbuka ilikuwa Uingereza kipindi kile nilikuwa na shoo nchini humo.
“Nakumbuka
walinifuata watasha wengi tofauti lakini huyo mmoja alining’ang’ania sana
nipige naye picha.
“Kwa kweli alinilazimisha sana kwa sababu mwanzo nilikataa
lakini baadaye nikaona isiwe ishu nikampa ushirikiano alioutaka.
“Mimi sikuona
matatizo alivyotaka tusalimiane kwa kugusisha vidole kwa sababu nilikuwa sijui
chochote kuhusu Freemason. Nimeijua baada ya mambo haya kuyasikia kwa sana hivi
karibuni.
“Kwa hiyo inawezekana siku hiyo waliniunganisha bila mimi kujua
(kicheko).”
SASA UKWELI NI UPI?
Mara kadhaa Diamond amekuwa akihusishwa na Freemason kutokana
na mafanikio ya ghafla aliyoyapata na mvuto alionao kwa mashabiki wake ndani na
nje ya Bongo.
Ijumaa Wikienda lilipotaka kupata ukweli kutoka kwake, Diamond
alifunguka:
“Si kweli bwana, mimi nazisikia tu hizi habari kama wengine.
Nasikia tu ipo hapa Bongo na kiongozi wake ni Sir Andy Chande, zaidi ya hapo
sijui chochote.
“Mimi ni mtu wa swala tano na mafanikio yangu naamini Mungu
ndiyo kila kitu.”
KUNA MSANII MWINGINE
Mbali na mwigizaji Jacqueline Wolper na marehemu Steven Charles
Kanumba ‘The Great’ ambao wamekuwa wakitajwatajwa na mambo ya Ufreemason,
Ijumaa Wikienda limetajiwa msanii mwingine ambaye yupo mbioni kujiunga akidai
anakwenda kufuata utajiri.
AANZA
KUPATA MAFANIKIO
Msanii
huyo ambaye ni mwigizaji mwenye jina (tunalihifadhi kwa sasa) anadaiwa kuanza
kupata mafanikio ya ghafla hivyo Ijumaa Wikienda lipo mzigoni na litakapomuweka
kati litamrusha hewani.
No comments:
Post a Comment