Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman
Sigara Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi
kwa madaktari hao.
|
Wandishi wa habari wakiwa kazini.
|
Mkurugenzi wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr E.
Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya.
|
BODI ya
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 72 kwa kosa
la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya
mkataba.
Imeelezwa kuwa
madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka
miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya
afya.
Akizungumza na
waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman
Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni
ukiukwaji wa kanuni za utumishi wa umma toleo la 2009 kifungu namba F.16-F17 na
F. 27.
"Hivyo
kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri
wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za
kinidhamu,"alisema Sigara.
Kwa mujibu wa
Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15
waliokuwa zamu (Intern Doctors 12 na Registrars3) hawakufika kazini na tarehe
24/6/2012 wafanyakazi 19 (Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.
Alisema,
kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54 na
Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo tarehe
25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya
utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.
Sigara,
aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao
hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya
kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.
Alisema, baada
ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali iliwaandikia barua za
kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba
walioingia na hospitali na pia kukiuka kanuni za kudumu za utumishi wa umma
nalo walilikaidi.
"Iwapo
madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo tarehe
28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao
watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii,"alisema.
Aidha, alisema
kuwa kwa ujumla madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye
kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za
kisheria za kuwafukuza kazi.
No comments:
Post a Comment