May 9, 2012

WASHIRIKI WA BBA TOKA BONGO! HAWA HAPA...

Hilda na Julio wanahitaji kura zetu ilikubaki kwenye mjengo wa Big Brother 'StarGame' 2012. Tafadhali piga kura kupitia www.africamagic.tv/bigbrother  au tuma SMS na jina Hilda au Julio kwenda 15726.

Wawakilishi wa Tanzania BBA Julio na Hilda wakipozi!

Wawakilishi wa Tanzania Big Brother ‘StarGame’ 2012, Julio na Hilda wakitabasamu.


Hilda akihojiwa alipokua anaingia mjengoni BBA huku mwenzake Julio akitabasamu.





KITENDAWILI cha nani anaiwakilisha Tanzania kwenye kinyang’anyiro cha Big Brother ‘StarGame’ 2012, Jumapili iliyopita kiliteguliwa baada ya kutangazwa majina ya washiriki wawili, ‘mapatna’ Julio na Hilda.

JULIO
Julio Batalia ni Mtanzania, mkazi wa Dar es Salaam, mwenye umri wa miaka 27, akiwa na Shahada ya Uzamili katika mambo ya mahesabu.

Kwa mujibu wa Julio, alifikia hatua ya kuingia kwenye Big Brother StarGame kutokana na aina ya maisha yake na baada ya rafiki yake kipenzi, Hilda kuwa mmoja wa washiriki anayeamini atakuwa bora zaidi.

Julio alisema Hilda ni mrembo mwenye maisha halisi na siyo ya kuigiza hivyo huwa anapenda kuwa karibu naye muda wote.

“Yuko smati, anavutia sana, Afrika nzima itampenda mno,” alisema Julio akimzungumzia Hilda.

HILDA
Hilda ni Mtanzania, mkazi wa Morogoro mwenye umri wa miaka 28 akiwa ni mfanyabiashara mwenye mtoto mmoja wa kiume ambaye alivutiwa na Biggie mwenyewe (kaka mkubwa) kuingia Big Brother StarGame.
“Anaonekana ni mtu mwenye changamoto ndani ya mjengo hivyo nilijisikia furaha sana nilipochaguliwa kuungana naye kwani nataka changamoto zake,” alisema Hilda na kuongeza:

“Julio ni swahiba wangu mkubwa. Ni mtu mchangamfu, mzuri na mwelewa.”
Kwa mujibu wa Hilda, fedha watakazoshinda, yaani dola za Kimarekani 300,000 (takribani Sh. milioni 500) baada ya kukaa mjengoni kwa siku 91, watazitumia kusaidia makundi mbalimbali ya wasiojiweza kwenye jamii.

Washiriki hao wa Bongo, Julio na Hilda na wale wa Zimbabwe, Maneta na Teclar, tayari wamewekwa kwenye mstari mwekundu wa kuoneshwa mlango wa kutokea Jumapili ijayo hivyo kitakachowaokoa ni wapiga kura kupitia mtandao wa Big Brother Africa.                              Habari kwa msaada wa Internet.




























No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...