May 7, 2012

KESI YA LULU YASIKILIZWA TENA LEO MAY 7 OMBI LAKE LATUPILIWA MBALI...

Lulu akiingia Mahakamani kusikiliza kesi yake leo tarehe 7 Mai akiwa chini ya ulinzi mkali wa Askari Magereza.

Hapa akiingia Mahakamani Kisutu kusikiliza kesi yake inayohusiana na kifo cha Kanumba.
 _________________________________________________________________________

Msanii wa filamu za maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, leo amepandishwa tena kizimbani mara ya tatu katika kesi ya mauaji ya Kanumba inayomkabili ambapo mawakili wanaomtetea wakiongozwa na Kennedy Fungamtama waliwasilisha ombi la kurekebisha umri wa mshitakiwa huyo kuwa miaka 17 na si 18 kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.
Fungamtama na jopo lake walisema mteja wao ni mtoto mdogo hivyo kesi hiyo ipelekwe mahakama ya watoto na kuwasilisha cheti kinachoonesha ana umri wa miaka 17. Upande wa mashitaka umetupilia mbali ombi hilo na kudai cheti kilichowasilishwa kina mapungufu kadhaa likiwemo jina la Dyana ambalo halijawahi kusikika likitumiwa na mshitakiwa huyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...