May 24, 2012

UBINGWA WA SIMBA KUSHEREHEKEWA DAR LIVE JUMAPILI MAY 27. FAMILIA YA MAFISANGO KUPEWA PESA NYINGI NA SIMBA..

Kombe la Ubigwa wa Simba ambalo wapenzi watapata nafasi ya kupiga nalo picha siku ya sherehe hizo ndani ya Dar Live.

Kamwaga akiwa  na  kombe la ubingwa wa Simba.

Nahodha wa  Simba, Juma Kaseja,  akielezea  sherehe hiyo.

Mratibu wa Burudani wa Ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo (kushoto) akiongea na waandishi juu ya sherehe hizo.

Juma Kaseja akiwa na makombe mbalimbali ambayo Simba wameyatwaa miaka ya nyuma na sasa.

Waandishi wa habari wakiwa kazini katika hafla hiyo.
______________________________

KLABU  ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam imepanga kufanya sherehe kubwa ya kutwaa ubingwa wa soka wa Ligi Kuu ya Vodacom katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live siku ya Mei 27, Jumapili wiki hii. Akiongea na waandishi wa habari jana mchana Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga,  alisema kuwa wameamua kufanya sherehe hizo ndani ya ukumbi huo kutokana na ubora wake. Aidha Kamwaga alisema kuwa siku hiyo pia watawatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa kwa msimu ujao wa ligi na kuwataka wapenzi wa Simba  na wananchi wengine kujitokeza kwa wingi siku hiyo.


______________________________



Baada ya kutoka taarifa za kwamba wiki hi klabu ya Simba itafanya sherehe za kushangilia ushindi wa kombe la VPL baadhi ya mashabiki tofauti wamekuwa wakitoa maoni hasi juu ya uamuzi wa klabu hiyo kufanya hivyo wakati ikiwa imefiwa na mchezaji wao Patrick Mafisango wiki iliyopia tu. Hivyo leo kupitia mtandao wa Facebook msemaji wa simba alijibu maoni hayo kama ifuatavyo.

Ezekiel Kamwaga - Msemaji wa Simba
Nimesoma sana maoni ya watu kuhusu show ya Simba DarLive.... Nakubaliana na karibu wote waliotoa haki yao. Kwanza mimi ni nani au Simba ni nani hadi isikubaliane na maoni ya watu? Lakini ningependa kusema machache kuhusu maoni ya watu.... Mosi, watu wa mpira wanajua kwamba kuna kitu kinaitwa logical reason na footballing reasons. Kwamba kuna mahali inabidi soka ifanywe soka na logic ibaki kuwa logic. Ndiyo maana kuna msemo kwamba Common Sense Is Not Always Common. Nitafafanua....Alipokufa uwanjani Marc Vivien Foe miaka kumi iliyopita, pambano liliendelea kama kawaida.... It was not logical reason, it was footballing reason.... Mara baada ya kifo cha mchezaji Antonio Puerta wa Celta Vigo mwaka 2007, siku tatu baadaye Celta ilicheza na AC Milan, na ikatangazwa kuwa ni kwa heshima ya Puerta, hata kama kuna wachezaji walishindwa kucheza.... Footballing reason... Maisha si mali ya binadamu.... Hebu tuseme hivi, Kama Simba itasubiri hadi arobaini ya Mafisango ipite ndipo ifanye sherehe na kwa bahati tukapata msiba mwingine siku ya 35, je, itabidi tuahirishe tena kwa siku nyingine 40? Au Taifa likapata tukio ambalo litasababisha tuingie kwenye maombolezo, au Mungu apishilie mbali, itokee kitu kinaitwa Force Majeure kwa lugha ya kisheria (an act of God) kama vile tsunami au tetemeko la ardhi, tutafanyaje? Tutaahirisha tena? Kwa wanaomjua vema Mafisango, kama angeulizwa huko aliko (Mungu amweke mahali pema peponi) yeye angekuwa wa kwanza kuturuhusu tufanye sherehe yetu ya ubingwa.

Nimebaini kwamba wako watu ambao wanataka kuonyesha kwamba Simba haina huruma au haijaguswa kabisa na msiba wa Mafisango kuliko wao. Baadhi yetu tumeishi na Mafisango, tumelala naye, tumefanya naye mazoezi na tunamjua kuliko baadhi ya watu ambao wametoa comments... Sasa najiuliza, hivi mwenye uchungu na Mafisango ni nani haswa? Yule ambaye aliamka saa kumi alfajiri na kwenda Muhimbili kuhakikisha amehifadhiwa vizuri na kumuandalia msiba na mazishi ya kitaifa au yule ambaye analalamika tu kila kukicha? Simba ina uchungu sana na Mafisango lakini It is a football club na lazima maamuzi yake yana base kwenye football na si common sense au mila za kiafrika.

Kufanya sherehe kwenye mazingira haya ni kumuenzi pia Mafisango. Timu inachukuaje ubingwa na kukaa tu kana kwamba hakuna kilichofanyika? Tusisahau kwamba kinachofanyika mwaka huu ni kitu kipya... Hii itakuwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 75 ya Simba kufanyika Bus Tour.

Hii ni kama Pilot Project.... We can only get better....Mwakani, tutachukua on board yale mapungufu ya mwaka huu na kufanya kitu kizuri zaidi.... Lakini, mnaupondaje uongozi kwa kujaribu kufanya kitu kizuri... Mbona mwaka juzi hakuna miongoni mwenu aliyetoa wazo la Bus Tour? Kwanini Watanzania tumekuwa na tabia ya kutaka kuponda tu kila kitu badala ya kutoa maoni ya kurekebisha ili twende vizuri.

Kuna mtu hapa anaitwa Mohamed Mashango, naona yeye anajua kuponda tu....Anafikia hatua ya kulinganisha Simba na timu ya mtaani kwake ya Kitintale.... Haya ni matusi kwa Simba, lakini ndiyo aina ya washabiki wa Simba tulionao !

Simba haijui kufanya sherehe? Nani anafanyaga Simba Day kila mwaka? Ni klabu gani nyingine ina utaratibu wa kufanya kitu kama Simba Day katika ukanda huu wa Afrika Mashariki? Kuna klabu gani imewahi kufanya party ya kiwango cha juu hapa Tanzania kama wakati tunazindua Simba TV? Mashango anapata wapi ujasiri wa kuilinganisha Simba na Kitintale? Glorie namuonaga uwanjani na hata mazoezini wakati mwingine lakini sijui kama huyu Mashango anakuja hata mpirani.... Au anaangaliaga ya Kitintale?

Niwafahamishe pia kwamba mpango wa kusaidia familia ya Mafisango upo...Iwe kwa kuandaa mechi au namna nyingine yeyote.... Muhimu zaidi ni kwamba Simba itafiwa tena na tena. Na imewahi kufiwa huko nyuma pia.... Cha msingi ni kwa klabu kuweka utaratibu wa kusaidia familia za wachezaji wake wote katika siku zijazo... Hili ndilo klabu inalolipanga kwa sasa.... Lakini naomba niwaambie kitu kimoja, familia ya Mafisango itapewa fedha nyingi na Simba.... Kiasi ambacho hakuna klabu yoyote ya Tanzania au Afrika Mashariki imewahi kukitoa kwa familia ya mchezaji aliyefariki.

You can take my word on that..... Niseme mwishoni kwamba inawezekana ukumbi wa DarLive si mzuri, yes, we can take that on board.... Inawezekana washabiki hawajapenda kuweka viingilio, we can take that on board..... Pengine watu wangependa sherehe hizo ziandane na utoaji tuzo kwa wachezaji, hilo pia ni wazo zuri. Ninalichukua.

Ningetaraji michango ya namna hiyo kwa Wana Simba.... Si kusema hatujui kupanga sherehe, hatuna uchungu na Mafisango au tuna tamaa ya fedha.....

Ningeomba tushiriki kwenye sherehe za mwaka huu na tujiandae kwa sherehe nzuri zaidi, za kiwango zaidi na zenye ubora zaidi msimu ujao.... Hiyo ndiyo Simba.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...