Wastara |
Mke wa Sajuki (Wastara) ambae yuko India kwa sasa akiwa anamuuguza mumewe (Sajuki) amezungumza kwa mara ya kwanza na millardayo.com kuhusu hali ya sasa ya Sajuki.
Amesema “kwa kweli hali imebadilika na ninategemea kuona hali nzuri zaidi leo (Jana) ni siku ya tano toka tumekuja huku India, Sajuki amebadilika sana kwa sababu siku tulipoondoka Tanzania hali yake ilikua mbaya hata rangi alibadilika lakini kwa sasa amerudi kwenye hali ya kawaida”
Kwenye sentensi nyingine, Wastara amesema Sajuki alikua hawezi hata kuongea ukamuelewa, sasa hivi anaongea hata kwa mda wa saa moja kitu ambacho alikua hawezi kabisa na sasa hivi ameweza kukaa kabisa”

Sajuki alipokua akisafirishwa kwend |
Wastara amesema “changamoto tuliyonayo ni kwamba tunahudumiwa na watu mbalimbali ukiachana na dokta, hawajui kingereza sasa unaweza kukuta unahitaji kitu lakini hamuelewani, kitu kingine ni swala la chakula, chakula ni kipya kwetu wote wawili huku ni Asia wana vyakula vyao”
Kuhusu Ugonjwa wa Sajuki, Wastara amesema walivyoondoka Tanzania walijua wanakwenda India na Sajuki atatibiwa ugonjwa unaomsumbua moja kwa moja lakini kabla ya kufanyiwa chochote ikagundulika kwamba alikua na tatizo la pumzi hivyo haikuwezekana kutibiwa ugonjwa wake kwa sababu inatakiwa kabla ya kufanyiwa opareshen anatakiwa kuwa kwenye hali ya kawaida, kwa hiyo ametibiwa kwanza tatizo la pumzi ili aweze kuhema vizuri ndio aanze kutibiwa ugonjwa wake”
Kwa kumalizia Wastara amesema “mimi pia nilipofika tu India nilikua mdhaifu, nilipoteza Network zote ikabidi nilazwe kwa sababu nilikua hoi, hapa yenyewe nimelazwa lakini naendelea vizuri”
No comments:
Post a Comment