Apr 15, 2012

HAFLA YA TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS 2012 ZILIZOFANYIKA MLIMANI CITY DAR

Quen Darlin akifurahia Tuzo yake ya Mkali wa Dancehall mala baada ya kukabidhiwa na Mr Taji Liundi (Kushoto)
Mchekeshaji wa Ze Comedy Mr Mpoki akitambulisha moja ya kikundi cha kuburudisha

Waendeshaji wa Shughuli nzima walikuwa Milard Ayoo na Mdada Vanessa Mdee.

Muwakilishi wa Arusha Gold akipokea tuzo ya wimbo bora wa Ragga kutoka kwa Khadija Mwanamboka

Ali Kiba akikabidhiwa tuzo yake ya wimbo bora wa Zouk na Dina Marios pamoja na Rainfred Masako.

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul a.k.a Diamond  ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award 2012, baada ya kujinyakulia tuzo tatu. (Mtunzi Bora wa nyimbo, Video bora ya Mwaka –Moyo wangu na Mtumbuizaji bora wa kiume). “Namshukuru Mungu, wakati mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo nimeibuka  na tuzo tatu”,alisema.
Chid Benz akimkabidhi tuzo msanii Diamond ya mtumbuizaji bora wa kiume.
Diamond akipokea tuzo yake ya Mtunzi bora wa nyimbo kutoka kwa Meneja wa bia ya Kilimanjaro,Bw.George Kavishe.
Diamond akipokea tuzo yake ya Video bora ya Mwaka toka kwa Muigizaji/mchekeshaji Mahiri wa kikundi cha Vuvuzela Entertainment, Mr Evans Bukuku.


Ukumbi wa Mlimani City ukiwa umejaa wapenzi na Mashabiki wa Music siku ya utoaji wa tuzo ya Kilimanjaro Music awards 2012


*******************


Mbali na Diamond, msanii mwingine aliyebahatika kunyakua Tuzo mbili katika tuzo hizo ni Suma Lee aliyenyakua tuzo za WIMBO BORA WA AFRO POP ambao alipata kupitia wimbo wa HAKUNAGA na Tuzo ya pili ni ya WIMBO BORA WA MWAKA Ambao pia ni HAKUNAGA.

Aidha msanii Chipukizi wa Bongo Fleva, Omy Dimpoz nae ametamba baada ya kunyakua tuzo ya WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA wa  NAI NAI aliomshirikisha ALI KIBA na pia alitwaa tuzo ya MSANII BORA ANAECHIPUKIA kupitia wimbo wake huo huo wa NAI NAI.
 
Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa milimani alikuwa katika kundi hilo la wasanii wenye tuzo mbili baada ya kupata tuzo ya WIMBO BORA WA HIP HOP wa  MATHEMATICS na Tuzo ya MSANII BORA WA HIP HOP.

Wasanii na Vikundi vingine ambavyo vilijinyakulia tuzo ni pamoja na  WIMBO BORA WA RAGGAE Ulikuwa ni ARUSHA GOLD wa kundi la WARRIORS FROM EAST huku Tuzo ya WIMBO BORA WA DANCE HALL ukiwa ni MANENO MANENO wa QUEEN DARLIN.

Tuzo ya WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA ulienda kwa Ali Kiba kupitia wimbo wake maarufu wa DUSHELELE , Tuzo ya WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI ilikwenda kwa A.T kwa kibao cha VIFUU TUNDU.

Tuzo nyingine ilikuwa ni ya  WIMBO BORA WA TAARABU aliyonyakua mwana dada wa kikurya (Mkurya wa kwanza kuimba Taarabu) anaeimba Taarabu Aisha Mashauzi kupitia wimbo wa NANI KAMA MAMA wa kundi lake la Mashauzi Classic.

Kundi la Twanga Pepeta nalo lilijinyakulia Tuzo ya WIMBO BORA WA KISWAHILI kupitia wimbo wa DUNIA DARAJA 

WIMBO BORA WA R&B ukienda kwa Ben Paul kupitia wimbo wa NUMBER ONE FAN.

Tuzo nyingine katika mfululizo huo wa Kili Music Award 2012 ilikwenda kwa Kalijo Kitokololo aliyepata Tuzo ya RAPA BORA WA BAND ambapo Tuzo ya WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI ilienda kwa Wimbo wa KIGEUGEU uliyoimbwa nae JAGUAR.

Tuzo zingine ni za MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE iliyoenda kwa KHADIJA KOPA, tuzo ya  MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI (Producer) ilienda kwa MANEKE.

Tuzo ya HALL OF FAME ilienda kwa TAASISI JKT, Tuzo ya HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI ilienda kwa Mtu mzima KING KIKII na HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI Ilinyakuliwa na Hayati REMMY ONGALA.

Mkonngwe wa uimbaji wa nyimbo za Kibongo Judith Wambura Habash “Lady Jay Dee" alinyakua tuzo ya MWIMBAJI BORA WA KIKE huku kijana aliyeshika kasi kutoka kundi la THT Barnaba akifunga jahazi hilo kwa kunyakua tuzo ya MWIMBAJI BORA WA KIUME.

Wasanii wote tunategemea kupata vitu vikali zaidi ikiwa ni hatua nyingine ya kujiandaa katika tuzo za mwakani (Kili Music Awards 2013) Bidii yako ndo inayokufanya upate tuzo. Kazi kwenu!!!


 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...