Jun 19, 2013

Mh. Joseph Mbilinyi (Sugu) apata ajali.

Mh. Joseph Mbilinyi
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi amepata ajali katika eneo la kasheki wilayani Hanan'g akielekea Arusha mjini.

Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu alikuwa akielekea Arusha mjini kuungana na wabunge wengine wa Chadema katika shughuli ya kuaga marehemu waliolipukiwa na bomu kwenye mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika ajali hiyo hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa, Mbunge huyo yuko salama, gari la Sugu limeharibiwa vibaya baada ya kugongana na basi la abiria.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...