Jun 9, 2013

Stars yatibua safari ya Brazil

Ili kusonga mbele, sasa Taifa Stars italazimika kushinda mechi zake mbili za mwisho, dhidi ya Ivory Coast itakayochezwa Dar es Salaam, kabla ya kusafiri kwenda Gambia.

Taifa Stars, usiku wa kuamkia leo ilitia doa safari yake ya kwenda kucheza fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Marrakech, mjini hapa.

Katika mchezo huo, Stars ilihitaji ushindi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri, lakini ilijikifungwa mabao hayo mawili, moja katika kila kipindi, huku bao la kufutia machozi likifungwa na Amri Kiemba.

Matokeo hayo, yameifikisha Morocco pointi tano, lakini ikiendelea kubaki nafasi ya tatu, na Stars imebaki na pointi sita nafasi ya pili nyuma ya Ivory Coast iliyoifunga Gambia mabao 3-0 na kufikisha pointi 10.

Kipindi cha kwanza kilishuhudia Taifa Stars ikipelekwa puta na wenyeji wao waliotawala sehemu kubwa ya kiungo na hivyo kuruhusu mashambulizi mengi yaliyomnyima nafasi ya kupumzika kipa na nahodha Juma Kaseja.

Stars ilimtumia mshambuliaji mmoja mbele, Thomas Ulimwengu na kufanya mashambulizi ya kushitukiza langoni mwa wapinzani wao.

Morocco wangeweza kufanya matokeo kuwa tofauti katika dakika za 5, 9 na 13 kama siyo Yousef El Arab, Hermach na Barrada kushindwa kumtungua kipa wa Stars.

Stars uliyokuwa ikishangiliwa na mashabiki 300, walibisha hodi lango la Morocco dakika ya 20 baada ya beki Shomari Kapombe kumjaribu kipa wa Morocco, Nadir Lamyaghri kwa shuti la mbali lililopaa juu ya lango.

Dakika tano baadaye Ulimwengu, alikuwa kwenye wakati mzuri wa kuipatia bao Stars baada ya kupokea mpira mrefu na kukimbia nao mpaka ndani ya boksi la hatari lakini akapiga kiki dhaifu iliyodakwa na Lamyaghri.

Mfumo wa Stars kucheza kwa kujiami zaidi kuliko kushambulia uliendelea kuleta hali ya mashaka langoni mwao, ambapo dakika ya 38 Morocco walipata bao la kuongoza kwa kiki ya penalti.

Penalti hiyo iliyokwamishwa wavuni na Abderazak ilitokana na faulo ya beki wa Stars, Aggrey Morris aliyemwangusha ndani ya dimba la hatari mshambuliaji Issam el Edoua.

Morocco alitumia mwanya wa Stars kucheza pungufu na kufanya, ambapo mwanzoni mwa robo ya kipindi cha pili, waliongeza bao la pili kupitia kwa Yousef aliyepita katikati ya ngome ya Stars na kumpiga chenga Kaseja.

AKAMATWA KWA KUIBA STULI YA MWENGE WA UHURU

Mwenge wa Uhuru.
ARUSHA, TanzaniaJIJI la Arusha limeendelea kujijengea sifa ya kuwa moja ya maeneo yenye vituko, kufuatia kijana mmoja mkazi wa eneo la Phillips, kata ya Sekei jijini humo, Hamad Rashid (32) kukamatwa leo akiiba stuli inayotumika kuwekea mwenge wa Uhuru wakati mwenge ukiwa katika mbio zake mkoani Arusha.

Tukio la kuiba na kisha kukamatwa limetokea jana saa 11 jioni katika eneo la Sanawari Mataa eneo lililopangwa kwa ajili ya mkesha wa mwenge huo baada ya kukamilisha mbio zake na kazi ya kuweka mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kamanda wa polisi mkoa wa  Arusha Liberatus Sabas ameithibitisha kutokea tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi waliokuwa wakiulinda mwenge pamoja na kiti hicho.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...