ROKIM GRAPHICS
Pages
Home
Sikiliza Passion FM
Swaga Magazine
Albam
Kalenda za Passion FM
Jun 12, 2012
KESI YA LULU HADI JUNI 25 MAHAKAMA KUU
WAKILI mmoja wapo anayemtetea Elizabeth Michael Fulgence Massawe akimsalimia ' Lulu' kabbla Jaji Dk. Fauz Twaibu hajaingia Mahakamani katika Mahaka Kuu ambako kesi hiyo ilipigwa tena kalenda hadi Juni 25 mwaka huu. Pia Jaji Fauz amezitaka pande zote mbili yaani Wakili wa Serikali pamoja na Jopo la Mawakili wanaomtetea kupeleka vuthibitisho kuhusiana na umri wa Lulu Mahakamani hapo.
Hapa akificha sura akikwepa picha pia alisikika akiwaambia waaandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kuwa amechoka kupigwa picha.
Hapa Lulu na Askari Wanawake wa Jeshi la Magereza wakienda kupanda gari ambako mtuhumiwa anarudishwa rumande.
Kipindi hiki Lulu alikuwa na kazi moja tu... Mkono kichwani kukinga kamera zisimchukue!!!
MAHAKAMA Kuu kanda ya Dar es Salaam imewataka mawakili wa utetezi na jamhuri kuwasilisha uthibitisho kuhusu umri wa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ kabla ya kutoa uamuzi wake Juni 25, 2012.
Agizo la Mahakama hiyo lilitolewa jana na Jaji Dk. Fauz Twaib anayesikiliza madai ya utata wa umri wa msanii huyo nyota wa maigizo nchini.
Kabla ya kuahirisha kesi hiyo Jaji Dk. Twaib alizitaka pande mbili zinazobishana kupeleka vithibitisho vya hati ya kiapo cha cheti cha kuzaliwa ili kujiridhisha umri sahihi wa Lulu.
Kwa upande wake wakili wa mshitakiwa Flugency Massawe alidai mahakamani hapo kwamba hadi Juni 13 atakamilisha vithibitisho hivyo wakati wakili wa serikali Elizabeth Kaganda alidai kazi hiyo ataikamilisha Juni 22 mwaka huu.
Lulu anayetuhumiwa kwa mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu anadaiwa kuwa chini ya miaka 18 huku jamhuri wakidai kwamba mshtakiwa huyo ana zaidi ya umri huo.
Pamoja na Massawe mawakili wengine wanaomtetea msanii huyo ni Jacqueline Dimelo, Kennedy Fungamtama na Maico Kibatala huku Shadrack Kimaro na Kaganda wakiongoza kesi hiyo upande wa jamhuri.
SERENGETI YAENDELEZA KAMPENI KUDUMISHA MILA NCHINI KWA KUDHAMINI MSIMU WA MAVUNO KWA KABILA LA WASUKUMA (BULABO)
Mgeni rasmi mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina akifungua rasmi mashindano ya ngoma za msimu wa mavuno kwa kabila la wasukuma (Bulabo) katika viwanja vya Red Cross kijiji cha Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya SBL, Ephraem Mafuru akishiriki kuzindua mashindano hayo yanayoshindanisha vikundi vya ngoma Wagika na Wagaru vya kabila hilo, katika kuadhimisha na kusherehekea mavuno kila mwaka, ambapo vikundi 30 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza zimethibitisha kushiriki.
Kundi hili la Makirikiri ya Shinyanga lilicheza ngoma kwa mvuto na style ya kipeke hivyo kuvutia wengi.
Hapa ngoma imepambamoto…
Ni Burudani kwa kwenda mbele!
Kundi jingine, Si katika bongo fleva pekee hadi ngoma asili kuna wasafi aka 'masharobaro'.
Ngoma za Bulabo zilianza mnamo mwaka 1700 kabla ya kuboreshwa na kuingizwa katika Kanisa Katoliki mwaka 1954, ambapo ngoma hizo za asili zilichezwa na kushindanisha makabila ya Wagika na Wagalu.
Kikundi kingine.
Chekshia engo adimu.
Ngoma tamu!! Kikundi kingine hapa…
Wacha wee!! Watu wamejipanga bwana.
Ngoma za utamaduni za asili ya kabila la Wasukuma ‘Bulabo’, zimepata udhamini wa sh. milioni 12 kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia ya Serengeti.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya SBL, Ephraem Mafuru alisema udhamini huo ni kwa ajili ya kuwezesha washiriki wa tamasha hilo la ngoma za asili za Bulabo mwaka huu.
Namna hii ili kunasa matukio kwa utamu....
Tunasubiri zamu yetu... wadau wa vikundi vya ngoma.
Ngoma hizi zitadumu viwanjani hapa kwa muda wa siku 8 ambapo jumapili ndiyo siku ya fainali, mshindi atatangazwa na wananchi watachinja ng'ombe na wote kula katika viwanja hivi. Hasa ukizingatia kuwa Mh. Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete keshatoa ng'ombe 14 kwa ajili ya kunogesha sherehe "...hii usikose"
Watu Nyomi.
Usafiri wa kumwaga…
Newer Posts
Older Posts
Home
Subscribe to:
Posts (Atom)