May 28, 2012

MUNGU MKUBWA, SAJUKI AENDELEA VIZURI!!!

Sajuki akiwa amepumzika, pembeni ni mkewe Wastara Juma.
Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa hospitalini nchini India.

____________________________

HEBU mwacheni Mungu aitwe Mungu! Hatimaye habari njema kutoka katika Hospitali ya Saifee iliyopo jijini Mumbai, India anakotibiwa staa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ zinatia faraja kwa Watanzania.
ANYANYUKA KITANDANI, AONGEA
Habari hizo njema zinaeleza kuwa Sajuki aliyeambatana na mkewe, Wastara Juma na kaka yake, hatimaye ameweza kunyanyuka kitandani na kuongea tofauti na siku aliyoondoka Bongo na mwanzoni alipofikishwa hospitalini hapo.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu, Wastara alisema Sajuki alikuwa amepata nafuu na hali siyo mbaya kwani alikuwa na uwezo wa kuzungumza hivyo akampa simu ili azungumzie afya yake yeye mwenyewe jinsi anavyojisikia.
SAJUKI LAIVU
Sajuki alipopewa simu alianza kwa kuwashukuru wale wote wanaomuombea dua na kujitolea kwa hali na mali ili kuokoa uhai wake.
“Namshukuru sana Mungu naendelea vizuri. Nilichukuliwa vipimo na nikabainika kuwa na uvimbe mwingi sehemu mbalimbali tumboni.
“Madaktari walibaini kuwepo kwa uchafu kwenye mapafu. Mwanzoni waligundua nina tatizo la kupumua na kukaukiwa damu.
“Wamelishughulikia hilo kwanza na hapa nilipo nimezungukwa na madawa, kwa kweli najisikia nafuu,” alisema Sajuki kwa sauti ya kukwaruza.
MADAKTARI
Sajuki alisema alipokelewa vizuri lakini kabla ya kuanza matibabu ya uvimbe tumboni, madaktari walilazimika kumtibu kwanza tatizo la damu na pumzi hivyo matibabu ya kilichompeleka hospitalini hapo (uvimbe) yakawekwa pembeni.
WASTARA ATIA NENO
Kwa upande wake, Wastara alisema kuwa Sajuki alipaswa kupatiwa matibabu kwa wiki mbili ndipo warejee nyumbani lakini kwa hali halisi inaonekana watakaa zaidi kwani tayari wiki mbili zimekatika.
MATIBABU YAANZA
Wastara alisema kuwa baada ya kumalizika kwa tatizo la pumzi na kupungukiwa damu, madaktari wameanza vipimo vya tatizo la uvimbe na kusisitiza kuwa uzi ni uleule wa kumwombea mumewe ili arejee katika siha njema.
TUMEFIKAJE HAPA?
Sajuki alianza kusumbuliwa na uvimbe mwaka jana ulioanzia mkononi na baadaye ndani ya mwili kwenye ini na sasa madaktari wanasema siyo kwenye ini tu bali na sehemu nyingine tofauti za tumboni.
NENO LA MWANDISHI
Kama alivyosema Wastara, tuzidi kumuombea dua Sajuki ili arejee katika ulingo wa filamu aendelee kutuelimisha na kutuburudisha tunapokuwa majumbani mwetu.

Habari toka GP.

Taarifa ya SMZ ya matukio ya uvunjifu wa amani

Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.

Aidha, Serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka pale ambapo wana maoni yoyote kuhusu serikali wafuate taratibu zilizowekwa na serikali itakuwa tayari kuzungumza nao ili kuwa na mustakabali mwema katika nchi yetu. Vile vile, kupitia taarifa maalumu ya serikali iliyotolewa Aprili Mei mwaka huu serikali ilieleza wazi kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi na kuwataka wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya kutaka kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka huu 2012.
Taarifa rasmi ya serikali kwa wananchi kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani nchini
Itakumbukwa kwamba tarehe 25 Aprili, 2012 Kamati Maalumu ya Mawaziri ilikutana na viongozi wa jumuiya ya Uamsho, Maimamu na Masheikh kuzungumzia hali iliyojitokeza nchini katika kufanya mihadhara ambayo ilikuwa inaashiria uvunjifu wa amani.
Katika kikao hicho serikali iliwataka viongozi hao wanapofanya mihadhara na mikutano inayohusu masuala ya maoni ya katiba wafuate taratibu zilizowekwa kisheria.
Aidha, serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka pale ambapo wana maoni yoyote kuhusu serikali wafuate taratibu zilizowekwa na serikali itakuwa tayari kuzungumza nao ili kuwa na mustakabali mwema katika nchi yetu.
Vile vile, kupitia taarifa maalumu ya serikali iliyotolewa Aprili Mei mwaka huu serikali ilieleza wazi kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi na kuwataka wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya kutaka kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka huu 2012.
Kwenda kinyuma na sheria hii ni kosa la jinai na hivyo iliwataka wananchi wote kujiepusha na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na matakwa ya sheria.
Ndugu wananchi mbali na juhudi hizo za serikali bado wapo watu wachache wasioitakia mema nchi yetu na umoja uliopo wanaendeleza kwa makusudi vitendo vya kuvunja taratibu za sheria jambo ambalo limepelekea jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria.
Ndugu wananchi serikali imesikitishwa na vitendo vilivyojitokeza vya vurugu na uvunjifu wa amani ambavyo vimeelezwa kwa kina na jeshi la polisi iliyotolewa mapema leo tarehe 25.05.2012 na kamishana wa polisi zanzibar.
Kutokana na hali hiyo serikali inawahakikishia wananchi wote kwamba itaendelea kudhibiti vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria vinavyoashiria kuondolea nchi yetu amani na utulivu uliopo.
Ndugu wananchi serikali inawahakikishia wananchi kwamba jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua zifaazo ili kuwahakikishia usalama wa raia na mali zao unakuwepo na hali inaendelea kuwa shuwari amani na utulivu.
Ndugu wananchi bado serikali inasisitiza na kuwaomba wananchi wote waunge mkono juhudi za serikali na kuwacha kabisa kujiingiza katika vitendo ambavyo vinaashiria uvunjifu wa amani na utulivu katika nchi yetu.
Hivyo tunawaomba wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida na serikali itaendelea kuwahakikishia usalama wao.
Aidha serikali inawaomba wazazi kuwadhibiti vijana wao wasijiingize katika vitendo viovu na vurugu kwani jeshi la polisi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vitakuwa macho kupambana na vurugu hizo na vitendo vyote vya uvunjifu wa amani.
Kwa madhumuni ya kudhibiti amani na utulivu na usalama wa wananchi wetu serikali katika kipindi hiki itachukua hatua zifuatazo:
1. Inakataza mikusanyiko ya aina mbali mbali, maandamano, na mihadhara ya aina mbali mbali ambayo haijapata kibali cha serikali.
2. Serikali inaliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na kufanya fujo zilizotokea katika maeneo mbali mbali ya zanzibar
3. serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa amali zilizofanywa katika taasisi za umma, dini na mali za watu binafsi.
4. Serikali inawapa pole wananchi na taasisi zilizoathirika na vurugu hizo na kuwahakikishia kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika katiak kadhia hiyo.
Na mwisho tunawaomba wananchi kushirikiana na serikali kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale ambapo itaonekana zipo dalili za uvunjifu wa amani katika maeneo yao.
Ahsanteni
Nawashukuru kwa kunisikiliza.
Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.

VURUGU ZA ZANZIBAR UAMSHO WAKANUSHA KUHUSIKA NA UCHOMAJI WA KANISA.

Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo mtaa wa Kariakoo mjini Unguja limechomwa moto usiku wa kuamkia jana.
Gari la Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Bishop Dickoson Maganga lililochomwa moto katika eneo la Kariakoo nje ya kanisa hilo.
Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU), kikizunguka katika maeneo ya Michenzani kuimarisha ulinzi ambapo tayari jeshi la polisi limepiga marufuku mikusanyiko yoyote.
____________________________
Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh Abdallah Said Ali ambaye ni miongoni mwa wanaotafutwa na jeshi la polisi akizungumza na Radio DW asubuhi mapema kabla ya taarifa ya kutafutwa kwao kutolewa kwa vyombo vya habari.

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR
Tarehe 27MAY2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.
Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.
Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.
Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.
Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.
Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.
WABILLLAH TAWFIQ
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...