Mwenge wa Uhuru. |
Tukio la kuiba na kisha kukamatwa limetokea jana saa 11 jioni katika eneo la Sanawari Mataa eneo lililopangwa kwa ajili ya mkesha wa mwenge huo baada ya kukamilisha mbio zake na kazi ya kuweka mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas ameithibitisha kutokea tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi waliokuwa wakiulinda mwenge pamoja na kiti hicho.
Alisema tukio hilo lilitokea wakati mwenge huo pamoja na wakimbizaji wake kitaifa, kimkoa na viongozi wengine wakiwa katika harakati za usomaji wa salamu za utii kwa Rais, kabla ya kutangazwa ratiba ya mkesha.
Kamanda Sabas alisema kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo alionekana kwa muda mrefu akiwa anazengea gari lililokua limebeba kiti hicho cha akiba bila kujua kwamba kulikua na askari waliokua wakimfuatilia nyendo zake.
Alisema muda mfupi askari mmoja alimuona kijana huyo akisogelea zaidi gari na kuingiza mkono kisha kuchomoa kistuli hicho kwa lengo la kuondoka nacho ambapo alishuka na kuanza kunyang’anyana nae kiti hicho.
“Unajua ni ngumu hata kueleza maana mtu na akili zake anafanya kitu cha namna hiyo. Hicho kiti kilikua ni cha akiba na kilikua ndani ya gari la wazi la mamlaka ya maji ambalo ndani yake kulikua na askari ambae alimuona na hata alivyotakiwa kukiacha aliking’ang’ania na kuanza kunyang’anyana hadi askari wengine wakisaidiana na mgambo walipotokea”alisema Kamanda Sabas.
Alisema mara baada ya kukamatwa alihojiwa na polisi waliomkamata ambapo alijibu kuwa alikua anataka kukiangalia tu na haikua nia yake kukiiba na kuomba msamaha lakini, polisi wanaendelea kumuhoji ili kubaini nia yake hasa ya kukichukua kiti hicho, Huenda akafikishwa mahakamani kwa kutaka kuiba kistuli cha mwenge.
Chanzo: Michuzi
No comments:
Post a Comment